logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Mwanajeshi ajikwaa na kuanguka katika ikulu wakati wa ziara ya Mfalme Charles

Kisa hicho kilitokea wakati Mfalme Charles III alipotembelea ikulu ya Nairobi Jumanne asubuhi.

image
na Radio Jambo

Habari31 October 2023 - 10:25

Muhtasari


•Mwanajeshi huyo alionekana akitembea kwa haraka nyuma ya rais Ruto na Mfalme Charles kabla ya kisa hicho cha bahati mbaya kutokea.

•Mfalme na mke wake Camilla wako nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku nne iliyoanza rasmi Jumanne, Oktoba 31.

katika ikulu ya Nairobi mnamo Oktoba 31, 2023.

Mwanajeshi mmoja wa kike alijikwaa na kuanguka chini alipokuwa akitembea kando ya barabara za Ikulu ya Nairobi wakati wa ziara ya Mfalme Charles III na Malkia Camilla siku ya Jumanne asubuhi.

Katika video ambayo inasambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwanajeshi huyo ambaye hakutambuliwa alionekana akitembea kwa haraka nyuma ya rais William Ruto na Mfalme Charles kabla ya kisa hicho cha bahati mbaya kutokea.

Ni pale mwanajeshi huyo aliyekuwa amevalia mavazi ya kijeshi ya rangi ya kahawia alipomkaribia rais na mgeni wake mashuhuri ndipo alipoanguka chini na kuinuka haraka.

Rais Ruto, Mfalme Charles na watu wengine waliokuwa karibu walionekana wakitazama eneo la tukio lakini mwanajeshi huyo aliamka haraka na kuendelea na safari yake. Kofia yake ilidondoka alipoanguka lakini aliichukua haraka na kuivaa haraka.

Kisa hicho kilitokea wakati Mfalme Charles III alipotembelea ikulu ya Nairobi Jumanne asubuhi.

Mfalme na mke wake Camilla wako nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku nne iliyoanza rasmi Jumanne, Oktoba 31.

Ziara hiyo inalenga kusherehekea uhusiano mzuri baina ya Kenya na Uingereza na ushirikiano thabiti na mahiri wanaoendelea kuuanzisha.

Ndege ya Kifalme ya Uingereza ambayo ilikuwa imewabeba Mfalme Charles III na Malkia ilifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) dakika chache kabla ya saa tano Jumatatu usiku.

Mfalme na Malkia watazuru Kaunti ya Jiji la Nairobi, Kaunti ya Mombasa, na maeneo jirani


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved