logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanamitandao wafurahia huku Diana Marua akim'post binti ya Bahati na Yvette baada ya muda mrefu

Ilikuwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu ambapo Diana alishiriki picha ya Mueni kwenye majukwaa yake ya mitandao ya kijamii

image
na Radio Jambo

Michezo11 December 2023 - 08:53

Muhtasari


•Katika video hiyo, watoto watatu wa Bahati walionekana wakiburudika pamoja huku wakicheza na baiskeli za kuteleza kwenye bustani.

•Ilikuwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu ambapo Diana alishiriki picha ya Mueni kwenye majukwaa yake ya mitandao ya kijamii.

Makumi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameelezea furaha yao baada ya mke wa Bahati, Diana Marua kum’post mtoto wa kwanza wa mwimbaji huyo, Mueni Bahati kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.

Siku ya Jumapili, mwanavlogu huyo maarufu wa YouTube kupitia ukurasa wake wa Instagram, alishiriki picha na video za Mueni akicheza pamoja na watoto wake wawili wakubwa, Heaven Bahati na Majesty Bahati.

Katika video hiyo, watoto watatu wa Bahati walionekana wakiburudika pamoja huku wakicheza na pikipiki na baiskeli za kuteleza kwenye bustani.

"Tuko nje," Diana aliandika chini ya chapisho hilo.

Watoto hao watatu walionekana kuwa na furaha pamoja.

Baadhi ya wanamitandao ambao walifikiwa na chapisho hilo walikuwa wepesi kutoa maoni yao kuhusu chapisho hilo huku wengi wao wakionekana kumuangazia zaidi Mueni na pia jinsi watoto hao walivyoonekana kuwa na uhusiano mzuri.

Tazama maoni ya baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Kenya;-

Bahatikenya: Mimi nawatafutia pesa kwa jua kali nyinyi mnaenda kukulia kwa kivuli!

Sly.3334: Sasa wenye mlisema Mueni hakupostiwa na Diana wakati wa siku yake ya kuzaliwa nangoja maoni zenu.

Faigh.kauria: Mueni amekuwa mkubwa.

Angela_kerubo: Bora Mueni ana furaha, tuna furaha.

Ivy_ivvy: Diana ni mzuri.. kazi nzuri mama, tunakupenda.

Mimahmmbaga994170: Mueni dada mkubwa

s.t.a.t.o.y.a : Atleast leo umepost binti yetu wa kwanza.

Gra_cey: Mueni kamagrow.. Diana wewe ni mpendwa mzuri.

Chapisho la Jumapili, ilikuwa ni mara ya kwanza baada ya muda mrefu ambapo Diana alishiriki picha ya binti ya Bahati na ex wake, Yvette Obura kwenye majukwaa yake ya mitandao ya kijamii.

Kumekuwa na uvumi mwingi kwenye mitandao ya kijamii baada ya mama huyo wa watoto watatu kupunguza kumsherehekea hadharani Mueni na mamake mapema mwaka huu.

Hadi kufikia mapema mwaka huu, mke huyo wa Bahati alikuwa akionekana kuwa na uhusiano mzuri na mpenzi wa zamani wa mwimbaji huyo, Yvette Obura na binti yao Mueni. Mambo hata hivyo yalibadilika chini ya hali isiyoeleweka mapema mwaka huu wakati wazazi wawili wa Bahati walipokuwa wakisema kutokuwa katika maelewano mazuri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved