logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Komeni kufanya kampeini za mapema -MP Ngunjiri Wambugu

Komeni kufanya kampeini za mapema -MP Ngunjiri Wambugu

image
na

Yanayojiri02 October 2020 - 01:50
Wanasiasa wanaotaka kuwania  urais mwaka wa 2022 wanafaa kukoma kufanya kampeini za mapema na badala yake  waangazie maendeleo ili kutekeleza ahadi walizotoa kwa wapiga kura mwaka wa 2017

Mbunge wa  Nyeri Mjini  Ngunjiri Wambugu  jana amewaambia viongozi hao kwamba nafasi ya urais itakuwa  wazi mwaka wa 2022 na kwa sasa wanafaa kutekeleza majukumu yao .

“ Tuna rais aliye afisini hadi mwaka wa 2022 , kama tu msiovyoweza kumruhusu mtu kufanya kampeini za kiti change kwani nipo kama mbunge ,pia hapafai kuwa na kampeini za kiti cha urais’ amesema Wambugu .

Mbunge huyo amesema hawapingi wenzake katika chama cha Jubilee lakini anatawaka watii agizo la kinara wa chama Rais Kenyatta kukomesha kampeini za mapema .

Alikuwa akizungumza katika kanisa la  Nyamachaki PCEA  mjini Nyeri ambapo alisambaza  hundi za cheki zenye thamani ya shilingi milioni 27 .2 kwa wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu katika eneo bunge lake .

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved