logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama yangu aliaga baada ya kujifungua mapacha-Gloria Muliro

Mama yangu aliaga baada ya kujifungua mapacha-Gloria Muliro

image
na

Yanayojiri02 October 2020 - 05:29
Msanii wa nyimbo za injili Gloria Muliro alifunguka na kueleza jinsi mama yake mzazi aliaga dunia, na changamoto alizozipitia baada ya mama yake kuaga dunia.

Gloria alifahamika sana baada ya kutoa kibao chake  cha 'omwami' kuvuma na kuenea sana katika mitandao ya kijamii, Gloria ameimba nyimbo zake akiwashirikisha wasanii mbalimbali wa nchi ya Kenya.

Akiwa katika mahijiano na radiojambo alikuwa na haya ya kusema,

"Tangu utotoni mwangu nimepitia changamoto nyingi kwa maana si kulelewa na mama mzazi mbali nililelewa na mama wa kambo

Kawaida kama binadamu tunajua jinsi kulelewa na mama wa kambo vile hukuwa,kwa kweli changamoto ni nyingi na mateso, baba yangu alipooa mama wa kambo alienda kufanya kazi

Siwezi kumlaumu baba yangu kwa maana alikuwa anatutetea sana alipokuwa akirudi nyumbani." Gloria Alizungumza.

Si hayo tu alieleza sababu za mama yake kuaga dunia na kuwaacha yatima,

"Mama yangu alikuwa mja mzito, alipoenda hospitali aliambiwa ako na shida baada ya kujifungua alijifungua mapacha na akaaga dunia asubuhi hiyo

Mapacha hao walikaa kwa muda wa miezi sita na wakaaga dunia, mmoja alipokuwa akizikwa na kaburi yake kufunikwa kwa njia tatanishi huyu mwingine akaaga huo wakati." Alisema.

Gloria akiwa katika mahijiano alisema kuwa baba yake ilimbidi aoe mwanamke mwingine kwa ajili walikuwa wadogo na hakuna mtu yeyote angewaweza kuwakimu.

" Mama yangu wa kambo aliaga dunia sasa ni miaka mitano tangu aage." Aliongea Gloria.

Msanii huyo walitengana na mumewe  kwa sababu kadhaa kutokana na madai ya uaminifu kwa ndoa na mbali na changamoto hizo Gloria amekuwa akiendeleza kazi zake za Usanii kwa kutoa nyimbo za kumsifu Mungu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved