logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maskini hana chake! Mmiliki wa nyumba Kawangware atoa paa la nyumba baada ya mpangaji kukosa kumlipa

Maskini hana chake! Mmiliki wa nyumba Kawangware atoa paa la nyumba baada ya mpangaji kukosa kumlipa

image
na

Yanayojiri02 October 2020 - 07:17
Ruth Shiundu, mkaazi katika mitaa ya mabanda ya Kawangware jijini Nairobi amelazimika kulala nje baada ya mmiliki wa nyuma aliyokuwa anaishi kuamua kutoa paa la nyumba kwa kukosa kulipa kodi.

Mama huyo wa watoto wanne amesema amekuwa akilipa kodi hiyo tangu kuhamia kwa nyumba hiyo Desemba japo mambo yalibadilika baada ya serikali kufunga shughuli nyingi nchini.

“Nimekaa hiyo miezi yote wa nne sasa ndio landlord anaona sifai kwa sababu kazi sasa imedidimia, mimi nauzaga mitumba ambayo sasa watu hawanunui kwa sababu hawajui zimetoka nchi gani,” amesema Shiundu.

Jaribio lake la kutakata kupata usaidizi limegona mwamba hata baada ya kujaribu kumfikia chifu wa mtaa huo japo hakuna usaidizi ambao ameupata.

“Aliniambia tarehe kumi mwezi huu lazima niwe nimemlipa nilipokosa nikamwambia sijapata akaniambia sitaweza na siwezi kuvumilia ndio akaja na caretaker wake na grinder akakata mlango wote,” Ruth amesema.

Mwanawe kijana Nevili aliongeza kwa kusema

“Deni ile ambayo tuko nayo ni ya miezi miwili tukiwa kwa do jana ndio huyu dadangu alipiga simu akasema caretaker wamepanda huko juu na ngazi wanatoa paa tukifika hapa tukapata imeharibika. Alisema Nevili.

Kulingana na mamlaka ya takwimu za kitaifa yaani Kenya National Bureau of Statistics kupitia kwa ripoti yao ya Jumanne, asilimia 30.5 ya wakenya hawangeweza kulipa nyumba Aprili kutokana na mkurupuko wa corona.

Asilimia 21.5 ya wakenya hawana uwezo wa kujikimu kimaisha .

Huku asilimia 59.8  ya wakenya wakiwa na uwezo wa kulipa nyumba kama walivyokubaliana na mmiliki wa nyumba.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved