logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ilikuaje: Nilijipata kwenye chumba cha kuhifadhi maiti ilhali sikuwa nimeaga

Ilikuaje: Nilijipata kwenye chumba cha kuhifadhi maiti ilhali sikuwa nimeaga

image
na

Yanayojiri02 October 2020 - 08:25
Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa na Dennis Mwaura ambaye amepitia changamoto nyingi. Mwaura hakuzaliwa akitembea na vijiti vya kujisaidia ila aliumia alipokuwa anafanya mazoezi ya densi.
"Nimelelewa na nyanya yangu kwa maana wazazi wangu walitengana nikiwa mtoto mdogo, nilipokua nilianza kucheza nyimbo kanisani kama 'b boy' yaani kijana na kuonyesha ushupavu wake

Siku moja nikifanya mazoezi ya densi nilisikia uchungu kwa uti wa mgongo, nilienda nyumbani kesho yake nilienda kanisani lakini nilikuwa na uchungu mwingi

Nilitoka kanisani nikaenda nyumbani, niliomba Mungu anipe usingizi Mungu alisikia maombi yangu, nilipoamka nilikuwa najaribu kuchukua simu lakini mkono haukuwa unasonga

Baada ya muda pia nilisongesha miguu lakini haikusonga, hapo ndipo nilijua nimepooza hata miguu." Alieleza Mwaura.

Cha kushangaza ni kuwa baada ya kuamka haikuwa Jumapili bali alipomwambia rafiki yake amuonyeshe simu ni saa ngapi alipomuonyesha ilikuwa Alhamisi saa kumi na moja.

"Ni jambo ambalo liliniumiza sana, rafiki yangu aliyekuwa anavuta bangi aliambia jamaa zangu lakini hawakuchukulia kama ni jambo muhimu

Nilikaa kwa miezi mitatu kwa nyumba bila kupokea matibabu yoyote, baada ya kupelekwa hospitali nilikaa kwa miezi nane bila ya hata rafiki na jamaa kuja kunitembea

Hata mama yangu hakuja, mama yangu aliniacha tu hamna kitu chochote kilitokea kati yetu." Alizungumza.

Kuna wakati Dennis Mwaura alijipata kwenye chumba cha maiti sababu ni ipi? hili hapa jibu

"Nilipokuwa kwenye wadi nilikuwa natetemeka sana nilikuwa nafungwa kichwa ili nisianguke, siku moja vile madaktari huwa wanakuja kubadilisha awamu usiku mmoja watu kumi waliaga kwenye wadi yangu

Huyo daktari alikuja na kuniuliza mimi ni nani kwa maana sikuwa na watu wa kunitembelea, aliniambia kuwa ni mimi nilikuwa natoa watu kafara

Baada ya hapo walileta wagonjwa wengine bali waliaga na usiku huo, siku iliyofuatia walileta wahubiri ili waje kuomba walinitoa nguo na kubaki na kaptura

Siku iliyofuatia madaktari walikuja kuita majina ya wagonjwa kila mmoja alikuwa hai isipokuwa mimi, walitayarisha kila kitu nikapelekwa kwa chumba kidogo cha kuifadhi maiti

Niliamka nijifunike blanketi nilijipata niko uchi kumbe nilikuwa kwa chumba cha kuifadhi maiti, nilipoamka na habari kufikia yule daktari alisema kwa kimombo 'the devil has come again."

Kwa mengi zaidi tembelea mtandao wetu wa kijamii wa youtube.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved