logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maambukizi ya corona Afrika Kusini yafikia watu nusu milioni- Waziri wa afya asema

Maambukizi ya corona Afrika Kusini yafikia watu nusu milioni- Waziri wa afya asema

image
na

Habari01 October 2020 - 10:47
unnamed (33)
Hukju mataifa kote ulimwenguni yakiendelea kukabilina na virusi hatari vya corona,taifa la Afrika kusini sasa limesajili watu nusu milioni walioambukizwa gonjwa hilo hatari ,taarifa zilizodhibitishwa na waziriu wa afya wa taifa hilo Zwelini Mkhize.

Akitoa takwimu za kila siku kuhusiana na maambukizi ya virusi hivyo,Mkhize alitangaza visa vipya 10,107 vya maambukizi mapya ,takwimu zilizofikisha watu 503,290 walioathirika.

Aidha waziri huyo amedhibitisha watu 8,153 waliofariki kutokana na gonjwa hilo.

Afrika Kusini katika bara la Afrika ndilo taifa lilioathirika zaidi huku nusu ya idadi ya visa vilivyoandikishwa Afrika vikitokea katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika.

Vile vile ni taifa la tano kote ulimwenguni kwa idadi kubwa ya maambukizi baada ya mataifa mengine ya Amerika,Brazil,Russia na India.

Viongozi wa taifa hilo sasa wanasema idadi hya maambukizi inaondelea kuongezeka kwa kasi huku visa vingi vikisajiliwa katika mjio mkuu wa Pretoria.

Akizungumzia visa vipya vya maambukizi ,kiongozi wa taifa hilo Cyril Ramaphosa amewarai wananchi wake kuwa makini na kuheshimu vigezo vilivyowekwa na serikali.

"We have to continue to work together to reduce the number of new infections. As with many other countries across the world, we need to continually adjust the measures we take to prevent new outbreaks or to safeguard our health system", Ramaphosa


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved