logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uchawi tena? Amber Ray ajitetea baada ya picha yake akiwa kwa ‘mganga’ kutolewa

Picha ya Amber akiwa amebeba kuku wawili yamtia mashakani

image
na Radio Jambo

Yanayojiri22 October 2020 - 12:45

Muhtasari


 

  • Picha ya Amber akiwa amebeba kuku wawili yamtia mashakani 
  • Amejitetea lakini wengi hawamuamini 

 

Faith Makau  aayejulikana kwa mashabiki wake kama Amber Ray amejipata katika ndimi za wengi hivi karibuni hasa baada ya mpenzi wake wa zamani  Brown Mauzo kuanza mahusiano ya kimapenzi na  Vera Sidika

   Lakini  licha ya juhudi zake  kujaribu kuendelea na maisha yake bila kufuatiliwa  mama huyo wa mtoto mmoja amejipata tena  pabaya huku ikitolewa picha moja  inayomuonyesha akiwa ‘kwa mganga’ .

 Madai kama hayo sio mageni dhidi yake kwani wakati mmoja alidaiwa kujihusisha na mambo ya ushirikina wakati mke mwenza wake wa zamani    Aaliyah Zaheer,  alipoolewa na mfanyibiashara na mwanasiasa wa Kenya  Zaheer Jhanda.

 Mwanasosholaiti huyo  aliolewa kama mke wa pili wa mwanasiasa huyo wa Kisii  Zaheer kwa miaka mitatu  na wana mtoto wa kiume ,Gavin .

 Wakenya walimhoji kuhusu alichokuwa akifanya baada ya picha hiyo kumuonyesha akiwa amewashika kuku wawili na kufunikwa kitambaa .

 Lakini Amber alipata ujasiri wa kuyajibu maswali hayo  wakati shabiki mmoja alipotaka kujua mbona anatumia mambo ya ushirika .Faith alimuambia kwamba yeye katu hajawahi kushiriki mambo hayo

 Wengi hawakuridhika na jibu lake na akasema kwamba atapata muda baadaye kusema upand wake wa kisa  wakati mashabiki watakapokuwa tayari kumuamini .

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved