Rais Uhuru Kenyatta aliwasili katika ukumbi wa Bomas dakika chache kabla ya saa tano asubuhi.
Uhuru alilakiwa na naibu wake William Ruto, kinara wa ODM Rial Odinga, spika Ken Lusaka na waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i.
Ruto aliwasili katika ukumbi huo saa 10:30 baada ya kinara Raila Odinga kuwasili.
Wakenya wengi walikuwa njia panda endapo Ruto angelihudhuria hafla hiyo kutokana na msimamo wake dhidi ya ripoti hiyo.
Wakati Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Upinzani Raila Odinga walikabidhiwa rasmi ripoti hiyo katika Kisii State Lounge, Ruto alisusia hafla hiyo na kuhudhuria mazishi katika kaunti ya Uasin Gishu ambapo alikosoa ripoti hiyo.
Viongozi wa humu nchini wengi wamehudhuria hafla hiyo huku rais akitarajiwa kuongoza zaidi ya wakenya 6,000 walioalikwa kuhudhuria uzinduzi rasmi wa ripoti ya Mpango wa Maridhiano (BBI).