Zari Hassan Diamond Platnumz wameendelea kuzima mitandao nchini Tanzania baada ya Zari kuwaleta watoto wake ili kumuona baba yao na kila hatua wanayochukua imeteka nyara ndimi za wengi .
Diamond hajawaona wanawe kwamiaka miwili tangia mwaka wa 2018 wakati alipotengana na Zari na amekuwa akionyesha matamanio makubwa sana ya kuwaona watoto wake .
Ziara hiyo imefanyika baada ya Staa huyo kumtaka mpenzi wake wa zamani Zari kuja Tanzania kwa sababu ya shughuli zake nyingi na hangeweza kwenda Afrika Kusini kuwaona wanawe . Zari alitangaza ziara hiyo kwa kuweka picha wakiwa katika ndege ya Kenya Airways katika kurasa za mitandao ya kijamii za watoto wake .
Kulikuwa na shughuli nyingi katika uwanja wa ndege walipotua huku wanagabari wengi wakitaka kuwapiga picha na kuwahoji walipolakiwa na Diamond .
Diamond baadaye alionekena akiwapeleka Zari na watoto wake katika kila chumba cha kasri lake akiwaonyesha pia tuzo nyingi ambazo amejishindia katika fai ya muziki .
Katikia video nyingine ameonekana akiwachezea gita watoto hao huku Zari akiwa pembeni akiangalia kwa tabasamu . Wengi wanajiuliza iwapo Zari na Diamond wataweka kando fahari yao na kurudiana ingawaje wote wamekanusha hilo