Msaidi wa zamani wa Kevin Hart ameshtakiwa kwa kuiba zaidi ya dola milioni moja '$1m (£730,000) kutoka kwa nyota wa Marekani.
Dylan Jason Syer, ambaye alianza kufanya kazi kama muigizaji wa Jumanji mwaka 2015, anashutumiwa kwa kuthibitisha manunuzi ambayo yalikuwa ayajaidhinishwa kwa kutumia kadi ya Hart.
Anashutumiwa kufanya ulaghai huo wa malipo kati ya mwezi Oktoba 2017 na Februari 2019.
Kijana huyo mwenye miaka 29 ameshtakiwaa kwa madai ya uhalifu wa wizi wa fedha, wizi wa utamblisho na ulaghai.
Kama atakutwa na hatia , bwana Syer, kutoka kisiwa cha Long Island City mjini New York, atahukumiwa miaka 25 gerezani.
Mtuhumiwa huyo atarudi mahakamani Februari 17.
Wakili wa wilaya ya Queens ,Melinda Katz alisema mtuhumiwa alipata mwanya wa kutumia kadi ya muigizaji huyo lakini aliendelea kutumia kinyume kinyume na utaratibu mpaka kiwango kikafika kiasi hicho.
Bwana Syer anadaiwa kununua bidhaa mbalimbali ukiwemo mkoba wa Louis Vuitton na saa ya Patek Philippe.
Bi Katz alisema alikuwa anaweka picha ya vile alivyonunua katika Instagram.
Bi Katz alisema tukuo hili ni angalizo kwa kila mtu kufuatilia gharama na matumizi yake ya kadi ya mkopo na taarifa za kifedha , bila kutegemea mtu mwingine tu, ni suala ambalo linapaswa kufanywa na mtu binafsi pia.
Hart alipokea $39m (£28m) katika uigizaji wake, kwenye ucheshi na udhamini wa mwaka 2020, kwa mujibu wa Forbes.
Habari kwa hisani ya BBC