logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uhuru apandisha hadhi kambi ya jeshi ya Manda

Rangi ya urais ni heshima kubwa zaidi iliyopewa kitengo cha jeshi kwa utendakazi mwema na huduma ya kipekee kwa taifa wakati wa amani na wakati wa vita.

image
na Radio Jambo

Habari23 September 2021 - 12:19

Muhtasari


• Rangi ya urais ni heshima kubwa zaidi iliyopewa kitengo cha jeshi kwa utendakazi mwema na huduma ya kipekee kwa taifa wakati wa amani na wakati wa vita.

Rais Uhuru Kenyatta anapokelewa na waziri wa Ulinzi Monica Juma na Mkuu wa mkuu wa majeshi ya KDF Jenerali Robert Kibochi katika Kambi ya Navy, Manda Bay katika Kaunti ya Lamu Septemba 23, 2021. Picha: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa katika kaunti ya  Lamu siku ya Alhamisi ​​kuongoza shughuli ya kuikabidhi bendera rasmi na rangi ya urais kambi ya kijeshi ya wanamaji ya Manda ili kuipandisha hadhi kambi hiyo.

 

Rangi ya urais ni heshima kubwa zaidi iliyopewa kitengo cha jeshi kwa utendakazi mwema na huduma ya kipekee kwa taifa wakati wa amani na wakati wa vita. Rangi ya urais ni bendera  maalum iliyo na alama zinazohusiana na kitengo ambacho kinachukuliwa kama alama ya kitambulisho.

 

Hafla hiyo ni muhimu kwa kila kitengo katika jeshi la Kenya na inaandikwa katika historia ya kitengo hicho.

 

Kulingana na desturi za jeshi, sherehe nzima ni moja ya uaminifu uliopewa kitengo cha jeshi. Hafla hizi sana sana hufanyika siku ya Jamhuri na haijulikani ikiwa itarudiwa wakati wa sherehe kwenye uwanja wa Nyayo.

 

 Maafisa wanasema rangi zinawakilisha azma ya serikali.

 

Kulingana na maafisa, kupoteza rangi kunasababisha kuvunjika kwa kikosi au kitengo.

Kambi zote zinakabidhiwa rangi za urais na za kitengo.

 

Kawaida rangi ya urais hutolewa wakati kitengo kinaongoza hafla katika sherehe za kitaifa au wakati amiri mkuu wa jeshi au kiongozi wa nchi ya kigeni anapewa heshima na kikosi husika.

 

Rangi zote mbili za urais na za kawaida zinachukuliwa na afisa mteule na kusindikizwa na maafisa wawili waandamizi wasio na amri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved