logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mabunge yaidhinisha walioteuliwa na Rais wa PSC,NGEC

Nafasi hiyo iliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti Stephen Kirogo baada ya kuugua  mwezi Aprili

image
na

Dakia-udaku21 December 2021 - 09:13

Muhtasari


•Uteuzi wa Antony Mwaniki kuwa mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC)

•Kirogo alikuwa akihidhinishwa  na kamati ya Leba na Jamii inayoongozwa na Mbunge wa Mwea, Josphat Kabinga

Wabunge wa Bunge la Kitaifa na Seneti wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11

Wabunge wameidhinisha uteuzi wa Antony Mwaniki kuwa mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).

Nafasi hiyo iliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti Stephen Kirogo baada ya kuugua  mwezi Aprili

Kirogo alikuwa akihidhinishwa  na kamati ya Leba na Jamii inayoongozwa na Mbunge wa Mwea, Josphat Kabinga.

Bunge linatarajiwa kujadili ripoti ya kamati baadaye siku  ya jumanne 21 ili kuunga mkono au kukataa uamuzi huo. Ikipitishwa majina hayo yatapelekwa kwa Rais kwa uteuzi rasmi.

Mabadiliko haya yamefanyika baada ya bunge kufanya makao maalum ambayo ya nia yake nikuzungumzia miswada inayohusiana na uchaguzi mkuu ujao  2022 pamoja na kuidhinishwa kwa uteuzi wa PSC.

Naibu wa Spika Moses Cheboi ndiye aliendesha shughuli hio muhimu ambapo alitangaza sababu za Spika kukosa kuhudhuria kikao hicho  cha wabunge

"Alipata ajali ndogo ofisini alipokuwa akijaribu kuvuta droo. Kiti chake kiliteleza na aliumia mkono wake wa kulia, bega na mgongo"Cheboi aliwatangazia wanachama kuwa spika alifanyiwa upasuaji mdogo na akashauriwa kupata nafuu nyumbani.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved