logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Huenda nitawania uwakilishi wa kike Nairobi - Shakilla

"Kwa sababu kila mtu anatuma maombi ya kuwania uwakilishi wa kike, huenda pia mimi nitawania kuwakilisha wanawake katika kaunti ya Nairobi,” amenadika Shakilla.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri04 February 2022 - 10:34

Muhtasari


• Mwanasosholaiti maarufu nchini Kenya, Shakilla amekuwa wa hivi punde kuibua tetesi za kuwa na ndoto ya kuwakilisha wanawake katika kaunti ya Nairobi.

• "Kwa sababu kila mtu anatuma maombi ya kuwania uwakilishi wa kike, huenda pia mimi nitawania kuwakilisha wanawake katika kaunti ya Nairobi,” amenadika Shakilla.

Mwanasosholaiti maarufu nchini Kenya, Shakilla amekuwa wa hivi punde kuibua tetesi za kuwa na ndoto ya kuwakilisha wanawake katika kaunti ya Nairobi.

Akiandika katika instastories zake, Shakilla amesema kuwa huenda atawania nafasi hiyo kwa sababu anaona ni kama kila mtu anaiwania pia.

Shakilla ambaye alipata umaarufu wakati kwa kipindi cha Wife Material kilichoasisiwa na mchekeshaji Eric Omondi ameandika maneno hayo huku wengi wakidhani ni mzaha wake.

“Kwa sababu kila mtu anatuma maombi ya kuwania uwakilishi wa kike, huenda pia mimi nitawania kuwakilisha wanawake katika kaunti ya Nairobi,” amenadika Shakilla.

Mwanasosholaiti huyo aliibuka kuwa mada ya kuzungumziwa haswa mwaka 2020 aliposema kwamba ana umri wa miaka 19, tamko lililomkaribishia mmasimango na kejeli kutoka kwa watumiaji wa mitandaoni waliomwambia kuwa anadanganya.

Shakilla ni mmoja wa watu wenye umaarufu nchini Kenya ambao ni watata mno, itakumbukwa kuna wakati aliibua madai ya kufanya ngono na baadhi ya wasanii mashuhuri nchini Kenya na hata akawaorodhesha na kukataa kata kata kuomba radhi alipotakiwa kufanya hivo.

Kama kweli atawania uwakilishi wa kike Nairobi, Shakilla atakuwa anakipiga dhidi ya muigizaji wa kipindi cha Maria, Dorea Chege ambaye mwishoni mwa Januari alitangaza pia kuwania nafasi hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved