logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilipatwa na msongo wa mawazo baada ya kuambiwa kipindi cha Tabasamu kimekamilika-Muigiza Minnie Kariuki afunguka

niliigiza kwa miaka 4, nakumbuka tukipigiwa simu na kuambiwa Tabasamu imekamilika,

image
na Radio Jambo

Yanayojiri07 February 2022 - 12:48

Muhtasari


  • Huku akizungumzia safari yake ya uigizaji, akiwa kwenye mahojiano, alisema kwamba alitaka kuwa wakili, ili kupigania haki za binadamu

Muigizaji na mjasirimali Minnie Kariuki alifahamika sana kupitia uigizaji wake katika kipindi cha Tabasamu kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Citizen.

Huku akizungumzia safari yake ya uigizaji, akiwa kwenye mahojiano, alisema kwamba alitaka kuwa wakili, ili kupigania haki za binadamu.

"Nikiwa shule ya upili nilitaka kuwa wakili, lakini nilijijua baada ya kutoka kidato cha nne kwani nilifanya vyema katika uigizaji

Katika uigizaji wa Tabasamu, niliigiza kwa miaka 4, nakumbuka tukipigiwa simu na kuambiwa Tabasamu imekamilika, nililia kwa sababu sikuwa na kazi nyingine

Nilipatwa na msongo wa mawazo kwa miezi 3, niliamua kuanza biashara na nilitamani kazi ya ujenzi," Aliongea Minnie.

Pia muigizaji huyo anaigiza katika kipindi cha Single-ish, na pia aiigiza katika kipindi cha 'My Empress' kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Maisha Magic East.

Kando na uigizaji wake Minnie ni mama na mke wa mtu, alisema kwamba hakuwa naataka kuandikwa ndio maana alianzisha biashara yake

Pia aliwshauri wanawake ambao wanawategemea wanaume, kuwa pesa za wanaume haziwezi kuwakimu maishani.

 

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved