logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa ahukumiwa kifo baada kumpora bosi wake 30,000, Kibera

Jamaa amehukumiwa kifo baada ya kumpora bosi wake shilingi 30,000, Kibera.

image
na

Yanayojiri22 February 2022 - 13:48

Muhtasari


• Mahakama moja mtaani Kibera imemhukumu kifo jamaa mmoja aliyemvamia bosi wake kutoka taifa la China na kumuibia pesa na simu kimabavu, katika jumba la makazi huko Kilimani.

• Akitoa ushahid wake, Chen Daisheng aliiambia korti kwamba uvamizi huo ulifanyika wakati alipokuwa akijiandaa kuingia kwenye lift, ambapo alimkuta Kubasu akiwa ndani tayari.

Clause Masika

Mahakama moja mtaani Kibera imemhukumu kifo jamaa mmoja aliyemvamia bosi wake kutoka taifa la China na kumuibia pesa na simu kimabavu, katika jumba la makazi huko Kilimani.

Robert Kubasu alihukumiwa Jumanne na hakimu mkuu Esther Boke baada ya upande wa mashtaka kutoa ushahidi dhidi yake.

Mwendesha mashtaka  Nancy Kerubo aliwaita mashahidi watano ambao walitoa uushahidi wao katika kesi hiyo.

Akitoa ushahid wake, Chen Daisheng aliiambia korti kwamba uvamizi huo ulifanyika wakati alipokuwa akijiandaa kuingia kwenye lift, ambapo alimkuta Kubasu akiwa ndani tayari.

“Nilipoingia kwenye lift nilimkuta Robert ambaye ni mwajiri wangu pale ndani na tukaka naye,” alisema Daisheng.

Daisheng alisema kwamba alishangaa na kushtuka wakati ambapo mfanyikazi huyo alianza kumvamia muda mchache baadaye.

“Nilifungua mlango wa sehemu hiyo na ghafla nikamuona Robert akitoa panga na kuanza kunitishia na kunitupia cheche kupitia lugha ambayo sikuelewa,” aliiambia mahakama.

Kubasu alimwambia baadaye alimtaka bosi wake kumpa shilingi 30,000 halafu akatimka mbio baada ya kupewa pesa hizo.

Kesi hiyo iliripotiwa katika kituo cha polisi cha kilimani na baadaye mshukiwa kukamatwa.

Kulingana na vyeti vya mashtaka, kisa hicho kilifanyika mnamo 25/9/2019 katika eneo la Silver harbor katika barabra ya Kindaruma, kaunti ndogo ya Gagoreti kusini.

Hakimu Esther Boke alisema kwamba hilo lilikuwa kosa kubwa kutokana na ushahidi uliotolewa huku akisema mshukiwa atachukuliwa hatua ya kisheria.

Boke alitoa hukumu ya kifo kwa Kubasu baada ya mwendesha mashtaka, Nancy Kerubo kuiomba mahakama kumchukulia jamaa huyo hatua kali.

Aidha mahakama ilimpa Kubasu siku kumi nne kukata rufaa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved