Mwimbaji wa injili Nicah the Queen alishaamua kabisa safari hii hataki kunyongonyea pindi anapochambwa na watu mitandaoni kama ilivyo kawaida ya watu wengi kutaka kujibizana na watu mashuhuri.
Mwanadada mmoja alimsimanga Nicah k kwa kujaribu kuanzisha ugomvi usio na tija na mwanamitindo Amber Ray wiki iliyopita
Akimjibu m, Nicah amempa jibu zito ambalo lilimkausha shabiki huyo asiwe na la kujibu tena.
Baada na Nicah kupakia video kwenye Instagram yake akitembea na kusema kwamba hakuwa anajua kama ingefika siku yeye kuwa na ujasiri wa kiasi hicho, shabiki huyo alidakia na kumrushia kejeli moja zito akidhani kwamba Nicah atanyongonyea lakini alikuwa amekanyaga pabaya.
Katika maoni yake, shabiki huyo alikuwa anamkejeli Nicah kwamba hakufaa kujilinganisha au hata kuanzisha ugomvi na Amber Ray na kumtamkia maneno mengine ya kudhalilisha mwili wake.
“Uyu ndio anashinda kiji-compare na Amber Ray vile mwili inatingika kama tinga tinga mzee lool,” aliandika shabiki huyo kwa jina Sandrah Sanchez
“Mwanamke ni kutingika jamani, ama unataka nikauke kama bouncer,” alijibu vikali Nicah the Queen.
Maoni hayo yalivutia watu wengi ambao bila shaka walimuona ndiye mkosa na Wakenya walivyokosa Subira na stara walimkomesha kwelikweli kwa niaba ya Nicah.
Lakini si vizuri kudhalilisha mwanamke kwa maumbile yake, haswa pia wewe ukiwa ni mwanamke.