Mwanaume mmoja mjini Nakuru amekata korodani zake kwa kutumia kisu cha jikoni katika jaribio la kujitoa uhai.
Kulingana na ripoti ya polisi waliofika kwenye eneo la mkasa, Waweru Njoroge mwenye umri wa miaka 56 alivizia jikoni na kuchukua kisu kujikata korodani zake wakati mke wake alikuwa anakoga bafuni.
Kwa bahati nzuri mkewe alisikia usiahi mkali kutoka na mwanaume huyo aliyekuwa akiungulia machungu ya kitendo chake na kwa usaidizi wa wahisani wema walimkimbiza hospitalini ambapo hali yake ilidhibitiwa.
Mwanaume huyo bado hajapata ufahamu dhabiti wa kuelezea polisi kiini cha kufanya kitendo hicho cha kujeruhi nyeti zake.
Katika siku za hivi karibuni tangu ujio wa janga la Corona, kumekuwa na mripuko mkubwa wa watu wanaojitoa uhai kwa njia mbalimbali tena za kushangaza.
Baadhi wanahisi wengi wametamauka na gharama ya juu ya maisha na bei ya bidhaa mbalimbali nchini ikiendelea kukwea mlima na kazi za wengi kukatika kutokana na makampuni mengi kupunguza wafanyakazi kwa kukosa faida ambapo uchumi ulilemazwa pakubwa na virusi hivyo vya covid-19.