logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Magoha: Nidhamu ni nguzo mihumu katika ufanisi wa mwanafunzi

“Inasikitisha sana kuona mtoto anauwa mzazi. Unashangaa mambo yalianza kuharibikia wapi,”Waziri alisema.

image
na

Yanayojiri22 August 2022 - 13:04

Muhtasari


• Amesema kuwa baadhi ya shule kama vile Kapsabet imeweka sheria inayowafanya wanafunzi kudumusha nidhamu na kufanya mambo kitaratibu.

Waziri wa elimu George Magoha

Waziri wa elimu Prof George Magoha amesema kuwa huu si wakati wa wanafunzi kuamrisha kile kitakachofanyika shuleni.

 

Magoha ambaye alikuwa akizindua  programu ya kuwatambua wanafunzi NEMIS katika  taasisi ya   kutathmini mtaalaKICD, amesisitiza umuhimu wa nidhamu  kwa wanafunzi huku akirejelea kisa ambacho mwanafunzi anatuhumiwa kumuua mama yake.

 

“Inasikitisha sana kuona mtoto anauwa mzazi. Unashangaa mambo yalianza kuharibikia wapi,”Waziri alisema.

 

Amesema kuwa baadhi ya shule kama vile Kapsabet imeweka sheria inayowafanya wanafunzi kudumusha nidhamu na kufanya mambo kitaratibu.

 

“Ukienda shule ya upili ya Kapsabet unafikiri uko katika kambi la jeshi. Kila kitu iko na mpangilio. Hii ndiyo nnia,hata shule za kutwa pia ziige huu mfano,”Magoha alisema.

 

Kapsabet ilirekodi matokeo mazuri katika mtihani wa kitaifa K.C.S.E.

 

Kadhalika amehakikishia washikadau katika sekta ya elimu kwamba NEMIS itaaendana na mtaala wa usamili na utendaji(CBC) na kwamba serikali imewekeza sana ili kuboresha elimu nchini.

“Msiwe na shaka. Serikali haikosi pesa . Ina kila namna ya kufanya ili kuhakikisha kwamba miradi imetekelezwa tena kwa wakati.

 

Ameiomba serikali mpya ilenge kumsaidia zaidi mtoto kutoka familia maskini kama alivyofanya katika awamu yake  ambapo alitangangamana na wanafunzi kutoka kwenye mitaa madongoporomoka ambao wamekosa ufadhili licha ya uwezo wao mkubwa katika masomo.

 

“Naomba serikali  mpya ijizatiti katika kuwafadhili watoto kutoka familia zisizo jiweza. Kwa fursa hii niliyopewa, nimeweza kutangamana nao na ninajua uwezo walio nayo,”Alisema.

 

Magoha ameshukuru kwa  kuwa na fursa kuhudumu katika serikali ya Jubilee kama waziri wa elimu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved