logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) "Pik Pik ponk" Moses Kuria amsuta wakili Otieno Willis kwa maneno hayo yake

“Iwapo ningekuwa nikipinga ombi langu pamoja na mawakili hawa walaghai watembea kwa miguu, ninajisikia furaha Mahakama ya Juu kufutilia mbali ombi langu,” Moses Kuria alisema.

image
na Radio Jambo

Makala31 August 2022 - 13:34

Muhtasari


• Moses Kuria alisema kwamab ana furaha mahakama ilifutilia mbali ombi lake kwa sababu hangeweza kujibizana na wakili kama huyo .

• Alimuita wakili Otieno Willis kama wa michongo.

Aliyeuwa mbunge wa Gatundu South, Moses Kuria sasa amepata muda wote kutupa kiazi moto kwenye mdomo wa wakili Otieno Willis alimaliza kutoa mawasilisho yake katika mahakama ya upeo kuhusu kesi muungano wa Azimio la Umoja One Kenya inataka ibatilishwe.

Otieno Willis alizua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana akitoa mawasilisho yake huku jasho linamtoririka kama mtu ambaye amebeba nanga huku akikwea mlima.

Akizungumza katika moja ya wasilisho lake, Willis alisikika akizungumza maneno yasiyoeleweka maana huku baadhi wakidai alichanganya lugha ya Dholuo, jambo ambalo liliwachekesha wengi.

Kwa upande wake, Kuria ambaye aliangushwa katika kinyang’anyiro cha ugavana Kiambu awali alikuwa amewasilisha ombi kwenye mahakama ya upeo akitaka maombi ya Azimio yanayolenga kubatilishwa kwa ushindi wa Ruto yatupiliwe mbali.

Ila mahakama hiyo badala yake ilitupilia mbali ombi hilo la Kuria.

Sasa Kuria amemchimba figisu na mikwara wakili Willis kwa kusema kwamba huyo ndiye mwanasheria wa hovyo kabisa ambaye kama ombi lake halingetupiliwa mbali angeaibika hata kumenyana naye kwenye jukwaa la mahakama ya upeo.

“Iwapo ningekuwa nikipinga ombi langu pamoja na mawakili hawa walaghai watembea kwa miguu, ninajisikia furaha Mahakama ya Juu kufutilia mbali ombi langu,” Moses Kuria alisema.

Wengi walizua gumzo kuhusu kutokwa kwake na kijasho kingi huku wakisema kwamba alipokea habari kura zilizotakiwa kuhesabika zimemalizika katika vituo 15 na hakuna kubwa lililobadilika, uvumi tu!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved