logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama Dangote amtangaza wazi mwanawe Tanasha Donna kuwa mrithi wa Diamond

Mr. Tom kaka mdogo leo namkabidhi kijiti cha wasafi 👬Mimi mwenyewe - Mama Dangote.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri26 December 2022 - 12:07

Muhtasari


• Mama huyo wa Diamond alipakia picha ya Diamond akiwa na mtoto wake Naseeb Junior na kusema amemkabidhi kijiti mwenyewe.

Mama Dangote amtangaza mwanawe Tanasha kuwa mrithi wa Wasafi

Bi Sandra ambaye ni mamake mzazi msanii namba moja wa muda wote ukanda wa Afrika mashariki kwa miziki ya Bongo Fleva Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa mtoto wa Tanasha Donna, Naseeb Junior ndiye rasmi mrithi wa Diamond Platnumz katika biashara ya Wasafi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mama Dangote alipakia picha ya Diamond akiwa na mwanwe huyo ambaye walizaa na Tanasha Donna wa Kenya na kusema kuwa rasmi amemkabidhi kijiti cha kuwa mrithi wa mwanawe Simba, Diamond Platnumz.

Mr. Tom kaka mdogo leo namkabidhi kijiti cha wasafi 👬Mimi mwenyewe,” Mama Dangote alitangaza bayana.

Wengi walifurahishwa na mfanano ulioko kati ya Diamond na mtoto wake Naseeb Junior huku wakisema kuwa uzuri wa baba umeonekana wazi kwenye panda la uso la mwanawe.

Tamko hili la mama Dangote linakuja wiki kadhaa baada ya sakata kuibuka mitandaoni kuwa mtoto wa Diamond na mwanasosholaiti Hamisa Mobetto si wake bali ni wa msanii mwenza BillNass.

Mtoto huyo wa kiume wa Hamisa Mobetto ambaye kila mtu anajua ni wa Diamond alionekana anafanana kwa ukaribu sana na msanii Billnass ambaye ni mume halali wa msanii Nandy.

Bilas haka ufichuzi huu japo haikuja kutoka kwa mtu wa kudhaniwa kuwa na ukweli ulionekana kutoa majibu ya ni kwa nini Diamond hajawahi mtakia mtoto huyo kheri njema wakati anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, kama anavyofanya kwa wanawe wengine aliozaa na Zari pamoja na huyu wa Tanasha Donna.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved