Huku mwaka wa 2022 ukiwa tayari umetamatika, nchini Kenya matukio yalikuwa ni mengi ambayo yalikuwa ni ya kuchosha akili.
Lakini pia kulikuwepo na watu wabunifu wa aina yake ambao waliibuka na misemo pamoja na memes mbalimbali ambazo zilihakikisha kwamba licha ya ugumu wa maisha ya ratiba nyingi za mishe mishe, watu walikuwa wanapata sababu ya kutabasamu na kucheka pindi tu walipokuwa wanaingia kwenye mitandao yao ya kijamii.
Katika Makala haya, tunakuandalia baadhi ya misemo ya utani, memes na vichekesho ambavyo vilifana na kuwaunganisha wakenya mwaka uliopita.
- Murife don’t run
Huu ni msemo ambao ulianza kusambazwa vikali ambapo mwanamke mmoja alisikika akimwambia mwanaume kwa jina Murife kutokimbia.
Kutokana na kile ambacho wengi walielewa, Murife licha ya kuambiwa asihofu wala kukimbia, alikaidi amri hiyo na balada yake kutumia ifaavyo falsafa ya ‘miguu niponye’
Wengi walitumia kichekesho hicho kuashiria ukinzani uliopo baina ya kitu na uhalisia wa kile kinachotokea badala yake.
2 Mapema ndio Best
Huu ni msemo ambao pia uliwaunganisha Wakenya pakubwa na ambao unakisiwa kuanza wakati wa kuwarai wakenya kuchukua kura kwa mapema ili kuzuia mkanyagano unaoshuhudiwa dakika za mwisho.
3 Kata simu tupo site
Mzee mmoja wa jamii ya Kisomali pia naye aliwafurahisha Wakenya kwa msemo huu ambao ulitumiwa na wengi kuonesha kuwa hawakuwa wametebwereka tu bali walikuwa na shughuli nyingi za kufanya na hivyo kuwataka watu kupunguza mawasiliano nao.
4 Sina maoni
Kijana mmoja kutoka kaunti ya Uasin Gishu ambaye alitrend baada ya kuulizwa maoni yake wakati wa uchaguzi lakini akasema kwa utani kuwa ‘Kwa maoni yangu mimi sina maoni’
5. Thank you very important
6. Ni bururi ugikuru
7. Enda usikie vibaya na huko
8. Huo ni uongo bana
9. Hii imeenda
10. Mambo ni mengi masaa ndio machache
11. Zoea hiyo sauti
Miongoni mwa nyingine. Wewe unakumbuka gani, au yako ni gani?