Mwanamume mwenye umri wa miaka 71, ameripotiwa kufariki akiwa na msichana wa miaka 22 katika chumba cha kukodi cha wageni maarufu Guesthouse au ukipenda lodging kwa lugha ya kimombo.
Mzee huyo aliripotiwa kukodi chumba kwa muda mfupi akiwa na kidosho mbichi mwenye umri wa miaka 22 ambaye alimchukua kutoka eneo la Githurai viungani mwa mji wa Nairobi.
Wawili hao baada ya kuingia chumbani, walianza shughuli zao hadi pale msimba ulipotolea katika kile wengi wanahisi kuwa huenda mzee alizidiwa na mbio za langalanga za kidosho huyo.
"Marehemu alianza kulalamika kwa maumivu ya kifua, mgongo na miguu na mikono kufa ganzi," polisi walisema katika ripoti yao kama ilivyonukuliwa na jarida moja la humu nchini.
Hapo ndipo mwanamke huyo aliposimamisha teksi kumpeleka mzee hospitali.
Kwa mujibu wa polisi dereva wa teksi, ambaye anafahamika sana na mwanamke huyo, alisaidia kumpeleka mzee huyo katika hospitali ya Aga Khan ambapo alitangaza kuwa amefariki alipofika.
Baada ya hapo ndugu wa marehemu aliarifiwa kuhusu kifo hicho.
Polisi walisema mwili huo haukuwa na majeraha yoyote ya kimwili hata kama wapelelezi walianza uchunguzi wa tukio hilo.
Tangu wakati huo wapelelezi wametembelea chumba hicho cha kulala wageni ambapo waliwahoji baadhi ya wafanyakazi waliokuwa zamu wakati wanandoa hao walipopanga chumba chao.