Kiongozi wa Azimio Raila Odinga amesema wanafikiria kufanya maandamano huku mazungumzo yakiendelea.
Akizungumza Alhamisi wakati wa bazara ya umma, Raila alikiri kuwa Rais William Ruto hakujitolea katika mazungumzo hayo.
Alikuwa akijibu wito wa baadhi ya viongozi, wafuasi na washikadau wakati wa kongamano hilo kwamba maandamano hayo yaendelee.
“Mazumgumzo iendelee na maandamano sambamba...dawa ya moto ni moto, kwa hivyo tunaendelea,” alisema Raila.
Alisema atatangaza hatua inayofuata baada ya mwisho wa Ramadhani.
Raila alisitisha maandamano baada ya wito kutoka kwa baadhi ya maaskofu na viongozi wenzake.
Ramadhan inaisha Aprili 21.