logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Aki rosecoco wewe!" Hisia mseto huku Willy Paul akimsamehe Miss P na kurudiana naye

Miss P aliomba msamaha kwa kudai Willy Paul alimlazimisha kushiriki mapenzi mara kadhaa miaka miwili iliyopita.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri22 April 2023 - 12:15

Muhtasari


•Siku ya Ijumaa, Willy Paul alichapisha picha nzuri yake na Miss P na kuonyesha upendo mkubwa kwa malkia huyo.

•Miss P alibainisha kwamba anajuta kuzungumza vibaya kuhusu Willy Paul wakati wa mahojiano ambayo alifanya awali

Ni wazi kuwa bosi wa Saldido International Willy Paul na msanii wake Miss P wamesuluhisha mzozo wao na wamerudiana baada ya miaka miwili.

Siku ya Ijumaa, mwimbaji huyo wa nyimbo za mapenzi alichapisha picha nzuri yake na Miss P na kuonyesha upendo mkubwa kwa malkia huyo.

"Unashika ni kama unaimiliki kwa sababu unaimiliki!" Pozee aliandika chini ya picha iliyomuonyesha akishika kiuno cha Miss P.

Mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili pia alichapisha picha yake nyingine na kipusa huyo na kukiri kumpenda.

"Nakupenda" aliandika.

Kama ilivyotarajiwa, mamia ya Wakenya ambao wanafahamu jinsi uhusiano kati ya wawili hao umekuwa kwa miaka iliyopita walikusanyika chini ya chapisho hilo ili kutoa maoni yao kuhusu maendeleo ya hivi punde.

Watumiaji wengi wa mtandao waliwapongeza wasanii hao wawili kwa kurekebisha uhusiano wao huku baadhi yao wakionekana kushangazwa na jinsi mambo yalivyoenda kasi katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Chris Kirwa: Hakuna kinachozidi mapenzi ya kusuluhisha. Inakuwanga moto sana mtu wangu.

DJ SHITI COMEDIAN: Sasa hii ni Hiit baada ya hiit.. Naumweke kejani awe anakupikia supu ya Kamongo.

VDJ JONES: Pampers zimepita thao kwa kweli

Mochere_3 Aki rosecoco wewe!

Rono: Watu huwa hamsomi!

Safari ya kurejesha uhusiano mzuri kati ya wawili hao ilianza mapema wiki jana baada ya Miss P kumuomba msamaha bosi huyo wake katika Saldido  kwa kumchafulia jina kwa madai mazito takriban miaka miwili iliyopita.

Hivi majuzi, Miss P akizungumza na Nicholas Kioko aliomba msamaha kwa Willy Paul kwa mambo yote aliyosema kumhusu.

"Willy Paul unajua tulikuwa na historia, yametokea mambo mengi ambayo sisi sote hatujivunii. Ni miaka miwili imepita na si vizuri kuelendelea kubebeana chuki kwa sababu inachosha,” Malkia huyo alisema.

Miss P alitaja msukumo wa nafsi yake kama sababu kuu ya kumchafulia jina Willy Paul takriban miaka miwili iliyopita.

"Ukiona hivyo nitajaribu kukutafuta lakini ukiona unaweza kufikia kabla sijafanya"

Aidha, alibainisha kwamba anajuta kuzungumza vibaya kuhusu Willy Paul wakati wa mahojiano ambayo alifanya awali

Huku akijibu msamaha wa Miss P siku moja baadaaye, Willy Paul alisema kuwa bado hakuwa na uhakika kuhusu kumsamehe.

Willy Paul hata hivyo alieleza kuridhika kwake kuona kwamba ukweli wote hatimaye umeweza kujitokeza.

"Miss P, siku zote kuna mwanga mwisho wa handaki. Ukweli huwa unajidhihirisha hata ichukue muda gani. Imepita miaka miwili ya maoni yasiyofaa kutoka kwa macho ya watu, sijui nisamehe au... " alisema kwenye Instagram.

Bosi huyo wa Radido International aliambatanisha ujumbe huo na video ya msanii huyo wake wa zamani akiomba msamaha.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved