logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Paula wa Kajala ni chakula changu, kiuno chake kinanitamanisha sana!"- Marioo

Paula alivunja uhusiano wake na Rayvanny mwaka jana.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri04 May 2023 - 04:44

Muhtasari


• Marioo alimsifia Paula baada ya kupakia video yake Instagram akicheza densi.

Marioo akiwa na muhibu wake Paula.

Huba la msanii Marioo na Paula wa mwigizaji Kajala Masanja linazidi kukolea munyu katika kila sekunde iendayo kwa Mungu.

Wawili hao ambao walianza kama mchezo tu wengi wakikisia ni kiki za kutoa wimbo wa Marioo ambao Paula alionekana, lakini ni kama wanataka kukiuka misemo ya watu na kuzama kabisa katika huba zito.

Marioo alimwahi Paula miezi kadhaa baada ya kuvunja uhusiano wake na msanii mwingine, Rayvanny na walitambua mahaba yao mitandaoni siku chache baada ya Rayvanny kurejea kwa mpenzi wake wa zamani Fahyvanny ambaye tayari wana mtoto mmoja pamoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marioo alipakia video ya Paula akinengua kiuno kwa taratibu na kusema kwamba hicho ni chakula chake anachokiona na kinamtamanisha mara kwa mara.

Marioo aliongeza makopa kuwa Paula ni kama kitumbua chake kizuri ambacho kamwe hawezi shiba akikila.

“Nyie mnaona mtu ana slay, Mimi nakiona Chakula changu kama iknantamanisha hivi  Aloooooo kweli Tunatofautiana kwenye kuona. Snack yangu ️‍🔥 @therealpaulahkajala,” Marioo aliandika akionekana kumshambulia Rayvanny kuwa alichokiacha ndicho yeye amekiokota na kukifanya kiwe cha thamani.

 Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na uvumi kuwa Rayvanny na Marioo wana chuki ambayo imeoteshwa na Paula, hata hivyo hilo halijawahi kuzungumziwa wazi na wasanii hao.

Licha ya kuendelea kuoneshana mahaba, bado asilimia kubwa ya watu mitandaoni wanahisi ni kiki Marioo na Paula wanafukuzia kwa kujaribu kuuza biashara zao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved