logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mlinzi amuua mwenzake kwa bunduki baada ya mabishano kuhusu ni wapi gari litaegeshwa

Watu walisikia mabishano na muda mfupi ikafuatiwa na milio ya risasi.

image
na Radio Jambo

Makala14 May 2023 - 06:33

Muhtasari


• Mlinzi huyo mtuhumiwa alichimba mitini na polisi walianzisha msako dhidi yake.

Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro

Mlinzi mmoja katika kampuni ya kibinafsi ya ulinzi mjini Kampala yuko mbioni baada ya kudaiwa kumpiga risasi mwenzake na kumuua katika nyumba yao ya kupanga eneo la Kalule, Parokia ya Lukuli, Tarafa ya Makindye, vyanzo kadhaa vya habari nchini humo vimeripoti.

 John Mujumbi, mlinzi mwenye umri wa miaka 25 anayehusishwa na Capital Guards and Patrol alidaiwa kupigwa risasi na mwenzake na mwenzake, Peter Ochoroi, 26, mwendo wa 12:30pm kufuatia kutoelewana siku ya Jumamosi kuhusu maegesho ya magari.

Wawili hao walikuwa katika kampuni moja ya ulinzi na wamekuwa wakishiriki chumba cha kukodi kilichotolewa na mwajiri wao.

"Walinzi wote wawili walikuwa na bunduki za SAR, kila moja ikiwa na risasi tano. Jukumu lao lilikuwa kutoa usalama katika vyumba vya IDAK huko Konge wakati wa usiku, kulingana na maagizo ya msimamizi wao,” naibu msemaji wa polisi, ASP Luke Owoyesigyire alinukuliwa na jarida hilo.

Walioshuhudia waliambia polisi kwamba walisikia mabishano kati ya walinzi hao wawili, yakiendeshwa kwa lugha wasiyoielewa na muda mfupi baadaye, mlio wa risasi ulisikika ukitokea katika chumba kimoja.

"Polisi walijibu haraka eneo la tukio, wakiandamana na timu ya tarafa na eneo la maafisa wa uhalifu. Mwathiriwa alikimbizwa mara moja katika Hospitali ya Mulago, ambako alitangazwa kufariki alipofika,” ASP Owoyesigyire aliongeza.

Tukio hilo linaripotiwa wiki moja baada ya tukio sawia la mlinzi kumshambulia bosi wake ambaye alikuwa waziri wa leba wan chi hiyo, Okello Engola.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved