logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zuchu kimemramba! Mashabiki wasema Diamond akionekana na mrembo uchi kochini

Kila mmoja sasa anasubiri kuona Zuchu atajibu nini kuhusu video hiyo ambayo imesambaa.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 July 2023 - 08:44

Muhtasari


β€’ Diamond alionekana anamshika shika makalio mrembo huyo ambaye alikuwa nusu uchi na kumlalia kifuani katika video hiyo ambayo imewagawanya wanamitandao.

Diamond achoma picha kwa Zuchu akionekana na mwanamke mwingine.

Mashabiki wamefurika mitandoani kumfariji Zuchu baada ya mpenzi wake Diamond Platnumz kuonekana na mrembo asiyetambulika wakiwa wamebarizi kwenye kochi.

Diamond alionekana anamshika shika makalio mrembo huyo ambaye alikuwa nusu uchi na kumlalia kifuani katika video hiyo ambayo imewagawanya wanamitandao.

Wengine walisema kwamba Zuchu hafai kuona video hiyo na kutaka msanii huyo asifikishiwe habari hizo, huku wengine bila huruma wakimtag kwenye chapisho hilo na kumcheka.

“Slide ya mwisho Zuchu hajaona,” mmoja alisema.

Ila braza si vizuri unavyomfanyia Zuchu kwenye hiyo slide ya mwisho... kumbuka naye ana moyo wa nyama,” mwingine alidakia.

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚iyo ya mwisho kuna mtu anaenda kuvunja vyombo uko leoπŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚ya mb zako,” mwingine alizua utani.

“Bro muda unaenda oa kaka πŸ˜‚”

Ikumbukwe hii si mara ya kwanza Diamond anaonekana kumkwaza Zuchu kwa makusudi kimapenzi baada ya wawili hao awali kuweka wazi kwamba walikuwa wanatoka kimapenzi licha ya kuwa na uhusiano wa Bosi na mfanyikazi.

Mwezi Mei baada ya kutoka kwa sehemu ya pili ya filamu ya uhalisia ya Netflix, Young Famous & African, Diamond alionekana akimla denda mwanasosholaiti kutoka Ghana, Fantana jambo ambalo lilimkwaza Zuchu.

Zuchu baada ya kuona kipande hicho wawili hao wakibusiana na hata Diamond mwenyewe kumsifia Fantana kwa ustadi wake katika kubusu, aliandika maneno ya kebehi yaliyolenga kwa bosi wake akisema;

“Mwambieni nilisema f***k you”.

Lakini pia itakumbukwa Zuchu mwenyewe aliweka wazi kwamba amemalizana kimahusiano na Diamond na uhusiano pekee uliosalia ni ule wa kufanya kazi chini ya lebo yake tu.

Diamond anaonekana na mrembo huyo asiyejulikana siku moja baada ya kupakia klipu iliyotoa sababu kwa nini amechagua maisha ya ukapera licha ya kuwa na kila kitu, lakini pia na watoto wanne kutoka kwa wanawake tofauti.

Kila mmoja sasa anasubiri kuona Zuchu atajibu nini kuhusu video hiyo ambayo imesambaa.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2026. All rights reserved