logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jaji aliyesimamisha utekelezwaji wa Sheria ya Fedha ahamishwa katika mabadiliko ya hivi punde

Nafasi yake itachukuliwa na Jaji Chacha Mwita katika mahakama ya Milimani.

image
na

Burudani08 August 2023 - 13:43

Muhtasari


• Jaji David Majanja amepelekwa katika Kitengo cha Kiraia kutoka wadhifa wake katika Kitengo cha Biashara na Kodi. 

Jaji Mugure Thande aliyesimamisha kwa muda utekelezwaji wa Sheria ya Fedha ya 2023 Rais William Ruto ni miongoni mwa majaji 13 waliohamishwa katika mabadiliko ya hivi punde katika idara ya mahakama. 

Mugure amehamishwa hadi Mahakama ya Malindi katika mabadiliko yaliyofanywa na Jaji Mkuu wa Mahakama kuu Jaji Eric Ogola. Nafasi yake itachukuliwa na Jaji Chacha Mwita, ambaye atakuwa Jaji mkuu katika Kitengo cha Katiba na Haki za Binadamu cha Milimani. 

Mwita aliwahi kuhudumu Malindi hapao awali.Jaji Diana Kavedza ataongoza mahakama mpya maalum katika Mahakama za Kibra na Kahawa.  Kwa sasa ametumwa katika Idara ya Uhalifu ya Milimani. 

Jaji David Majanja amepelekwa katika Kitengo cha Kiraia kutoka wadhifa wake katika Kitengo cha Biashara na Kodi. 

Katika mabadiliko hayo, Mahakama Kuu ya Nakuru itaongozwa na Jaji Hedwig Ong'undi wa Kitengo cha Katiba na Haki za Kibinadamu huko Milimani.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved