logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Serikali kuongeza vituo vya matibabu ya kansa katika kaunti nne

Tayari kuna vituo katika kaunti za Mombasa, Nakuru na Garissa ambavyo zinafanya kazi

image
na Brandon Asiema

Yanayojiri22 November 2024 - 15:39

Muhtasari


  • Kuongezwa kwa vituo hivyo kunalenga kugatuliwa kwa huduma ya matibabu ya kansa, kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa na kuimarisha ufikiaji wa matibabu kwa jamii zote nchini.
  • Vituo hivyo vipya vitajiunga na vituo vilivyopo kwa sasa katika kaunti za Nakuru, Mombasa na Garissa ambavyo tayari vinatoa huduma kwa wagonjwa wa saratani.

caption

Kenya inapania kuongeza katika siku za hivi karibuni kufungua vituo vingine vinne vya matibabu ya kansa katika maeneo tofauti tofauti nchini.

Waziri wa afya Deborah Barasa, amesema kuwa serikali itapanua huduma kwa wagonjwa wa saratani kwa kuongeza vituo vya saratani vya kikanda katika kaunti za Kisumu, Kakamega, Meru na Nyeri. Waziri amesema hayo kwenye mkutano wa nane wa mkutano wa kimataifa wa saratani wa Kenya jijini Kisumu.

Kwa mujibu wa waziri Barasa, vituo hivyo vipya vitajiunga na vituo vilivyopo kwa sasa katika kaunti za Nakuru, Mombasa na Garissa ambavyo tayari vinatoa huduma kwa wagonjwa wa saratani.

Kuongezwa kwa vituo hivyo kunalenga kugatuliwa kwa huduma ya matibabu ya kansa, kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa na kuimarisha ufikiaji wa matibabu kwa jamii zote nchini.

Katika hafla hiyo, waziri Baraza amesisitiza kujitolea kwa serikali katika kudhugulikia ongezeko la ugumu wa matibabu ya saratani kupitia uwekezaji wa miundombinu sahihi, utambuzi wa ugonjwa huo na ujumuishaji wa huduma chini ya mpango wa huduma ya afya kwa wote UHC.

Vile vile, Barasa amesema kuwa matibabu ya saratani yamejumuishwa katika mfuko wa bima ya afya ya jamii chini ya mamlaka ya afya kwa jamii SHA ili kupunguza mzigo wa kulipia huduma hiyo kwa wagonjwa.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved