Naibu wa rais aliyeng’atuliwa mamlakani Rigathi Gachagua ameendeleza shutma dhidi ya rais William Ruto akimhusisha na matatizo yanayoshuhudiwa nchini shutuma za kurejea kwa pombe haramu ambapo watu watatu waliripotiwa kufa baada ya kubugia pombe katika eneo la Lanet, kaunti ya Nakuru.
Akizungumza katika ibaada ya kanisani mjini Naivasha, Gachagua amemlaumu rais William Ruto kwa kukosa kuendeleza kampeni dhidi ya pombe haramu tangu ang’atuliwe mamlakani huku akimshutumu kwa kuruhusu machifu na polisi kuacha kupigana dhidi ya pombe hiyo haramu haswa katika eneo la mlima Kenya.
Gachagua amemsuta rais kwa kuruhusu pombe haramu katika eneo la mlima Kenya jambo ambalo amelitaja kuwa nia ya kuwamaliza vijana na eneo hilo ili kupunguza idadi ya wapiga kura wa ukanda huo wa kati wa Kenya akitaja kuwa kinyume cha maadili na jambo lisilokubalika kulenga jamii.
“Tangu wanitoe kwa kiti ile pombe yote mbaya ya kuua watu rais aliagiza iletwe hapa kwa mlima imalize vijana wetu. Na ni kinyume cha maadili, ni jambo lisilokubalika kulenga jamii kwa uharibifu na sumu.” Alisema Gachagua katika ibaada ya kanisa la PCEA mjini Naivasha.
KiongozI huyo wa zamani katika utawala wa Kenya Kwanza, mbali na kulalamikia kulegea kwa vita dhidi ya pombe haramu, ameisuta serikali kwa kukosa kukamilisha miradi ya maendeleo kama vile usambazaji wa umeme, miradi ya ujenzi wa barabara na maji akitofautiana na miradi ya ujenzi nwa nyumba ya bei nafuu.
Mbunge huyo wa zamani wa Mathira aameshangazwa na namna Wakenya watafika kwenye nyumba hizo za bei nafuu ikiwa hamna miundo m,binu msingi ya usafiri ambayo ni barabara.
“Hakuna hata moja umemaliza, Barabara zimesimama, maji imesimama, stima
imesimama wewe unasema unataka kujengea watu manyumba, sasa hii manyumba kama
hakuna barabara watu watafika wakipitia wapi? Alisema Gachagua.
Hata hivyo Gachagua amemtaka Rais kuacha hasira
na kurejea kwa watu na kufanya mazungumzo namna alivyojitokeza na Bibilia wakati
wa kampeni akiomba kura.