logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hakuna usajili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza tena, CBC imeshika kasi

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, hakutakuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule za sekondari.

image
na OTIENO TONNY

Yanayojiri06 January 2025 - 10:10

Muhtasari


  • Shule zikifunguliwa kote nchini madarasa za kidato cha kwanza zitasalia bila wanafunzi  baada ya mtaala mpya ya elimu ya CBC kushika kasi.
  • Wanafunzi ambao walikalia mtihani wao wa kitaifa katika mwaka wa 2023  walikuwa kundi la mwisho la 8-4-4 kufanya mtihani wa KCPE na kuhamia shule ya upili.


Shule zinapofunguliwa kote nchini madarasa za kidato cha kwanza yatasalia bila wanafunzi  baada ya mtaala mpya ya elimu ya CBC kushika kasi.

Shughuli za masomo zinaporejelea rasmi Jumatatu tarehe 6, Januari kwa mwaka 2025 historia itaandikwa  ambapo hapatakuwepo usajili wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza kwa masomoya sekondari chini ya mtaala wa 8-4-4. 

Wanafunzi ambao walikalia mtihani wao wa kitaifa katika mwaka wa 2023  walikuwa kundi la mwisho la 8-4-4 kufanya mtihani wa KCPE na kujuinga na shule ya upili, na pia watakuwa wa mwisho kumaliza cheti cha elimu ya sekondari ya Kenya (KCSE) mnamo 2027.

Serikali iko mbioni kutekeleza elimu inayozingatia umahiri (CBC) na kukomesha hatua kwa hatua mfumo wa 8-4-4 ulioanza mwaka 1985.

Mwaka mpya wa masomo unapoanza Jumatatu Januari 6, darasa la kwanza la CBC litakuwa linajiunga na  daraja la 9. Awali, shule za sekindari ya chini zilikuwa zikimilikiwa na shule za sekondari lakini kufuatia malalamiko na kero zilizotolewa na wadau mbalimbali wa elimu ilichangia kusalia kwa junior sekondari katika shule za msingi.

Uchagizo huu umesababisha mabadiliko makubwa kwani shughuli za kurudi shuleni zimekuwa tulivu kuliko kawaida. Wazazi wachache wameripotiwa kuzuru madukani kutafuta vifaa kama vile sare, vitabu na vifaa vingine vilivyozoeleka kuhitajika na wanafunzi wa kidato cha kwanza.

Wachapishaji na maduka ya vitabu pia wanahisi matatizo ya kifedha. Awali, biashara hizi huona ongezeko la mauzo mwanzoni mwa mwaka wa masomo wanaposambaza vitabu muhimu vya marejeleo. Hata hivyo, mwaka huu, wanakabiliana na akiba isiyouzwa ya vitabu vya kiada vya kidato cha kwanza.

Taasisi ya ukuzaji mtaala ya Kenya (KICD) pia ilikanusha madai ya uhaba unaokaribia wa vitabu vya kiada, haswa kwa Darasa la tisa ikisistiza kuwa kuna idadi ya kutosha ya vitabu hata katika maduka.

Mwaka wa masomo unaahidi kuwa wakati mahususi katika mageuzi ya mfumo wa elimu wa Kenya, huku nchi ikikabiliana na mabadiliko ya mahitaji ya CBC.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved