logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Shughuli za elimu kote nchini zarejea rasmi kwa ratiba ya mwaka 2025 kuanzia Januari 6

Wizara ya elimu ilitoa mwongozo au ratiba ya namna shughuli hzio za elimu zitaensdeshwa katika shule zote nchini

image
na Brandon Asiema

Yanayojiri06 January 2025 - 10:55

Muhtasari


  • Wizara ya elimu ilitoa mwongozo ya namna shughuli hzio za elimu zitaensdeshwa katika shule zote nchini 


Shughuli za elimu zimerejea rasmi kote nchini kwa ajili ya ratiba ya mwaka mpya wa 2025 baada ya mapumziko ya muda mrefu wa takribani miezi miwili.

Ufunguzi tena na shule unasadifiana na kutolewa kwa matokeo ya tathmini kwa wanafunzi wa gredi ya sita iliyofanywa mwaka jana wanafunzi waliokalia tathmini hiyo wakitarajia kujua matokeo na ripoti ya jinsi walifanya tathmini hiyo.

Shule zinaporejelea shughuli zake mwaka huu wa 2025, tayari wizara ya elimu ilitoa mwongozo au ratiba ya namna shughuli hzio za elimu zitaensdeshwa katika shule zote nchini.

Katika ratiba ya mwaka huu, muhula wa kwanza utakuwa wa jumla ya wiki 13 kuanzia Jumatatu , Januari 6, 2025 hadi Aprili 4, 2025 ambapo ndani yake kutakuwa na muda mfupi wa mapumziko wa siku tano kati ya Februari 26 na Machi 2. Wanafunzi watakuwa na muda wa wiki tatu wa mapumziko ya mwisho wa muhula wa kwanza.

Muhula wa pili utang’oa nanga Aprili 28 na kukamilika Agosti mosiikiwa ni jumla ya wiki 14, sawia ikiwa na siku tano ya mapumziko ya kati ya muhula kabla ya mapumziko ya mwisho wa muhula yatakayokuwepo kwa wiki tatu kuanzia Juni 25 hadi Juni 29.

Muhula wa mwisho utaanza wakati wanafunzi watarejea shuleni kuanzia Agosti 25 hadi Oktoba 24 ikiwa ni jumla ya wiki 9 za masomo kwa muhula wa tatu. Tofauti na mihula mingine, muhula wa tatu utakosa pumziko fupi la kati kati wa muhula kwa kuwa mitihani ya kitaifa ya KPSEA, KILEA na KCSE itaandaliwa.


Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved