
Serikali kuu chini ya wizara ya usalama wa ndani inawataka wamiliki wa mitandao ya kijamii wote kuweka ofisi zao nchini na wazi kufikiwa kwa wakati wote.
Baada ya miezi ya malalamishi kutoka kwa viongozi wakuu serikalini kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii nchini, hasa miongoni mwa vijana wa rika wakiongozwa na kundi la Gen –Z . Serikali sasa imetoa maelekezo kwamba kila kampuni inayomiliki mitandao ya kijami iwe na ofisi yake nchini itakayofikiwa na wakenya.
Maelekezo haya mapya yanalenga kuipa serikali uwezo wa kufatilia kwa karibu shughuli zinazoendelezwa k wenye mitandao hiyo ya kijamii ili kuweka uwazi kwa watumizi wake.
“ili kuhakikisha majukumu na uwazi hasa kutokana na uvumi wa habari za uwongo, ukiukaji wa sheria za mitandao ya kijamii pamoja na matusi yanayowathiri watumiaji wengine. Kwa hivyo kila mitandao ya kijamii ni sharti waweke ofisi zao nchini na tuwe na uwezo wa kuzifikia,” ilisema wizara ya usalama wa ndani.
Sheria hii hasa inaelekezwa kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii kama vile “Meta” ambayo inamilikiwa na Mark Zuckerberg ambaye pia anaimiliki Facebook (ambayo ina watumizi bilioni 3.07 ulimwenguni) , mtandao wa Instagram (wenye watumizi bilion 2.4 duniani), vilevile mmiliki wa mtandao wa X ambao awali ulijlikana kama Twiter (Ukiwa na watumiaji milioni 600) ambao unamilikiwa na mtu Tajiri sana duniani kutoka Marekani Elon Mask.
Kampuni zingine ambazo pia zimeathirika na maelekezo haya ni pamoja na Kampuni ya TikTok ambayo pia itatakiwa kuwa na ofisi yao nchini.
Maelekezo haya yanakuja baada ya mkutano kati ya katibu mkuu wa wizara ya
usalama wa ndani Raymond Omollo, na kampuni za mawasiliana na wasimamizi wa
mitandaao ya kijamii.
Kulingana na matamshi ya wizara ya usalama, sheria hizo zinatokana na kuongezeka kwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii miongoni mwa wakenya.
Matumizi mabaya yanajumuisha uchochezi ambao huenda ukaelekeza taifa pabaya, matamshi ya chuki kwa wakenya hasa viongozi.
Sheria hizi huenda zikarahisha matakwa ya serikali kukomesha matumizi mabaya ya miandao ya kijami, hasa baada ya waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen kuahidi kuongoza vita dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao na wataopatikana kuchukuliwa sheria kali pamoja na kufungwa hadi miaka mitano.
