Waziri wa teknolojia na mawasiliano William Kabogo amemwajiri Gen Z kwa jina Kennedy Maina kutoka gatuzi la Kiambu hii inafuatia hatua yake ya kukejeli mradi wa Kabogo wa WIFI ya bure kwenye masoko mbalimbali mtaani kwao, aliodai ni mradi ghushi na hautumiki kwa vyovyote vile.
Akiangika picha yake na ya Maina kwenye mtandao wake wa Facebook waziri Kabogo alisema kuwa anamhongera Maina kwa kujitolea kimasomaso na kuonyesha ukakamavu katika kuzungumzia suala hilo,vilevile waziri aliambatanisha arafa aliotumiwa na Kennnedy iliosheheni kejeli za kuusuta mradi huo wa WIFI ambao alidai hautumiki kabisa.
Katika ujumbe wake bwana Kennedy alisema kuwa amekuwa akifatilia kwa ukaribu semi ambazo waziri amekuwa akisema kuhusu kutoa Mitambo hiyo ya WIFI bure katika masoko mbalimbali akisema kuwa haikuwa ikifanya kazi bali ni maneno matupu.
''Hujambo ndugu jina langu ni Maina kutoka gatuzi la Kiambu tumeona na kukusikia ukizungumzia kuhusu kutoa huduma za mradi wa WIFI ya bure katika masoko mbalimbali yaliyoanzishwa na serikali kwa bahati mbaya inaonekana tu kimuundo bali haitumiki wala kutoa huduma yoyote''.
Kabogo alipousambaza ujumbe huo alisisitiza kuwa Kennedy hakukashifu tu miradi yake bali alileta mwanga na mwamuko mpya ndio maana niliamua kumuajiri kazi,akasisitiza kuwa kauli ya Kennedy ilikuwa ni pevu tena ya kufungua macho hivyo alipoupokea ujumbe kutoka kwake alipendezwa na maoni yake Kabogo alipousambaza ujumbe huo alisisitiza kuwa Kennedy hakukashifu tu miradi yake bali alileta mwanga na mwamuko mpya ndio maana niliamua kumuajiri kazi,akasisitiza kuwa kauli ya Kennedy ilikuwa ni pevu tena ya kufungua macho hivyo alipoupokea ujumbe kutoka kwake alipendezwa na maoni yake na akaazimia kumwajiri papohapo.
''Wazo ambalo Kennedy alitoa lilikuwa ni wazo zuri akisema kuwa WIFI ambayo imeratibiwa kutumika na Umma au katika sehemu za umma yafaa itumike na mtu kwa kulipia kiwango cha hela anazo tofauti na WIFI ambayo hutolewa kwa kampuni mbalimbali ambazo huwa ni ghali sana kuzilipia''hili lilikuwa wazo la Kenney kwa waziri Kabogo ambaye katika mtazamo wake alikuwa ameazimia kuzima mitambo hiyo yote.
Kabogo alikiri kuwa wazo la Kennedy lilikuwa zuri na kama wizara sasa wanalenga kuimarisha utendakazi na kutekeleza kila jambo ili kila kitu kiwe sawa kwani hii ni hatua muhimu na kwa hivyo wizara inapanga kuanzisha mradi mpana ambao utawajiri vijana wengi na kuimarisha hali zao za maisha hapa bwana Kennedy amenisalimi kwa uchanya 'nimesalimiwa positively' Kabogo alisema.