Mbunge wa Belgut Nelson Koech amedokeza kuwa waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi atafutwa kazi chini ya muda wa Juma moja au mawili yajayo.
Akizungumza wakati wa mahojiano mapema Jumatatau asubuhi ya Februari 3,2025 Koech ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya idara ya ulinzi ,ujasusi na na masuala ya jigeni amefichua kuwa Muturi yu njiani kuiga serikali.
''Waziri Muturi anamjaribu rais amfute kazi angekuwa amejiuzulu kitambo kama hataki kufanya kazi na serikali ameomba afutwe kazi na mtaona hilo kwa juma moja au mawili yajayo, amemchuna rais pua na kwa sasa yu njiani kuelekea nyumbani,'' Nelson alikariri.
Kauli hii inajiri muda mchache tu baada ya waziri Muturi kuzungumza na vyombo vya habari wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City mnamo Ijumaa Januari 31,2025 alipokuwa akizungumzia hali nyeti ya utekaji nyara wa vijana ambao umegeuka kuwa wa mauaji.
''Hili swala li katika uwezo wako bwana Rais wewe ndiye rais wa Jamhuri ya Kenya tena amri jeshi mkuu kwa hivyo ninamuomba rais ajitokeze amalize hivi visa vya utekaji nyara jinsi ulivyoahidi'' Muturi alisema.
''Lazima tume maalum iundwe ili ichunguze hii hali ili kubaini ni nini ambacho kinaendelea na ni nani ambaye anahuka katika suala hili hatuwezi kukubali suala hili liwe la kawaida',' Muturi alisema.
Bwana Muturi ambaye mtoto wake alitekwa nyara hatimaye alisema kuwa serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa inawajibikia hali hii kwa udharura unaostahili'.
''Ninamrai mheshimiwa rais kuamurisha kukomeshwa kwa haraka visa hivi vya utekaji nyara uliahidi wakenya kuwa visa vya utekaji nyara havitafanyika wala kutendeka kamwe chini ya utawala wako bwana rais hatuwezi kaa tukitazama hali hii ikiiendelea,"
Matamshi ya bwana Muturi yaliungwa mkono na Spika wa bunge la taifa Moses Masika Wetangula aliyesisitiza kuwa ni lazima visa hivi vichunguzwe na wale ambao wanafanya au kutekeleza mambo haya wakabiliwe vikali kisheria.
''Afisi ya mkurugenzi mkuu wa Ujasusi DCI afisi ya ya mkurugenzi na mwendesha mashitaka ya umma DPP na taasisi za usalama wa ndani wa taifa zifanye uchunguzi kwa kushirikiana na wahakikishe kuwa wanaofanya hayo mambo wanakamatwa.''Polisi wamekiri kuwa si wao wanaohusika katika vitendo vya utekaji nyara kwa hivyo wafanye uchunguzi wa kina ili kubaini ni kina nani hawa ambao wanatekeleza haya mambo kinyume cha sheria ili umma ufahamu kinachoendelea''.
.