KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 6.
Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za eneo la Mlima Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
KPLC walisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarbati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni Tharaka Nithi na Kiambu.
Katika kaunti ya Tharaka Nithi, baadhi ya sehemu za maeneo ya Giampampo na Rukindu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Sehemu za maeneo ya Kamwangi, Watathi, Mbichi, Wangige, na Gathiga katika kaunti ya Kiambu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.