KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Februari 18, 2025.
Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti 12 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, West Pokot, Uasin Gishu, Nandi, Kakamega, Homa Bay, Meru, Laikipia, Nyeri, Murang'a, Taita Taveta, na Mombasa.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Lang'ata Road, Kileleshwa, Dandora, Pipeline Estate na Amazon Pipeline zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Kapkoris na Chepareria katika kaunti ya West Pokot yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Outspan na Ancillia katika kaunti ya Uasin Gishu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Sehemu za maeneo ya Yala na Kaimosi katika kaunti ya Nandi zitakosa umeme kati ya saa tatu unusu na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Sigalagala na Musoli katika kaunti ya Kakamega yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za Oyugis, Nyangiela, na Ombek katika kaunti ya Homa Bay zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Maua na Garba-Tulla katika kaunti ya Meru yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Timau na Embori katika kaunti ya Laikipia pia yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Katika kaunti ya Nyeri, soko la Kiamabara litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja asubuhi.
Maeneo ya Kenol na Kimorori katika kaunti ya Murang'a yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za mji wa Mwatate katika kaunti ya Taita Taveta zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.
Maeneo ya Fort Jesus, na Mombasa Hospital katika kaunti ya Mombasa pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.