KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Februari 24.
Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kajiado, Nyeri, na Meru.
Katika kaunti ya Kajiado, sehemu za maeneo ya Ngong VET zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kinunga, Ihwa, Chania, na Soko ya Iruri katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Soko ya Igoji na Soko ya Kinoro katika kaunti ya Meru pia zitaathirika kati ya saa mbili na nusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.