IEBC itahijaji kitita cha shilingi 61.7bilioni kwa ajili ya kuandaa uchaguzi wa 2027, Obadia Keitany alisema
Kaimu afisa mkuu mtendaji wa IEBC Obadia Keitany siku ya
jumanne Februari 25,2025 alisema IEBC itahitaji shilingi bilioni 61.7 kwa ajili
ya uchaguzi wa 2027.
Alipofika mbele ya Kamati
ya haki na sheria katika bunge la taifa alielezea kuwa tume inalenga
kuwasajili wapiga kura wapya 5.7 kufikia mwaka wa 2027 ambapo idadi hiyo itawezesha
jumla ya wapiga kura kuwa 28m.
IEBC inapojianda kuteua makamishina wapya watakaojianda kwa
ajili ya uchaguzi mkuu ujao mamia ya wakenya walionyesha ari ya kutaka nafasi
hiyo na kufikia sasa jumla ya watu 1848 walituma maombi ya kuhitaji kazi hiyo.
Itakumbukwa kuwa mnamo mwaka wa 2021 aliyekuwa mwenyekiti wa
IEBC marehemu Wafula Chebukati alikuwa amependekeza kupewa shilingi bilioni
40.9 ili afanikishe uchaguzi ulio huru na wahaki wa mwaka wa 2022.
Wakati huo huo tume inapojianda na kuhakikisha kuwa makamishina
wanateuliwa na jopo kazi lililoteuliwa na hatimaye kuapishwa baada ya kupigwa
msasa na bunge la taifa watalazimika kuwa wepesi wa kufanya kazi ikizingatiwa
kuwa muda uliosalia ni mchache kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.
Kufikia sasa jumla ya shilingi milioni 481 zilikwisha tengwa
kwa ajili ya kushughulikia chaguzi ndogo
katika sehemu mbalimbali ambazo Wabunge,Madiwani,Mavana, Maseneta na Wawakilishi
wa kina mama kwa ajili ya kushughulikia chaguzi ndogo kutoka maeneo hayo.
IEBC inapojianda na kuratibu mipango na mikakati ya uchaguzi
mdogo na ujao rai zinazidi kutolewa kwa
tume hiyo kupewa muda mwafaka ofisini ili kuwe na umakinifu na mafunzo ya
kutosha kwa makamishina watakaoteuliwa.
Tume hiyo ya IEBC huhitaji jumla ya makamishina saba akiwemo
afisa mkuu mtendaji wa tume ambaye pia
hutumika ka sekritari wa tume.
Kumekuwa na shinikizo nyingi kutoka kwa Wakenya na Viongozi kwa
kutaka tume hiyo iunndwe kwa wepesi ili kurahihisha shughuli za uchaguzi na
kutimiza matakwa ya Katiba bila kuingia
katika migogoro ya kikatiba na kuvunjwa kwa sheria.
Kucheleweshwa kuundwa na kuwateua makamishina wa IEBC
kulitokana na kesi zilizokuwa zimewasilishwa
kortini kuzuia mchakato huo kuanza hadi kesi zisikilizwe na kuamuliwa,
lakini mapema mwaka huu korti iliondoa vizingiti hivyo na kuruhusu mchakato
rasmi kwanza.