
Kampuni ya Kenya Power imetangaza kuwa maeneo mbalimbali katika kaunti 10 yatakumbwa na katizo la umeme Jumanne, Machi 5, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, kukatika kwa umeme kunatokana na kazi za matengenezo ya mfumo wa usambazaji umeme. Maeneo husika yatakosa umeme kwa muda tofauti kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Nyandarua, Nandi, Tharaka Nithi, Kiambu, Vihiga, Laikipia, Meru, Mombasa, na Kilifi.
Nairobi
Baadhi ya maeneo jijini Nairobi yatakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo hayo ni:
Githurai 45: Co-op Bank, Naivas, Kingdom Sacco, Mt. Kenya, Kimbo, Mwana Mukia, Clanne Academy, Kassmatt, Fountain Junior, Kwa DO, Mukinye, Army Barracks, Sukari B, Mwiki School, Kimbo Police, sehemu ya Mwihoko, Farmers Choice, sehemu ya Clay City na wateja jirani.
Pipeline Estate na maeneo jirani: Jackmil Supermarket, Quick Mart Supermarket, PCEA Pipeline, Stage Mpya, sehemu ya Tassia Stage, Avenue Park 2 East, Kwa Kirima, Amazon, Pebble Hotel na maeneo ya karibu.
Lavington na maeneo jirani: Mageta Road, sehemu ya Mugumo Road, Ndoto Road, Lavington Shopping Centre, Isaack Gathanju Road, Maji Mazuri, Elmolo Drive, Lavington Curve, Shell Lavington, KFC Lavington, sehemu ya Muhoya Avenue, Jaffery Sports Club, Muthangari Road, Equity Lavington, Naushid Merali, Social House, Jacaranda Avenue, Ramisi Road, sehemu ya Gitanga Road, Maria Immaculate Hospital, Vanga Road, Masanduku Lane, sehemu ya Mbaazi Avenue, British High Commission Gitanga Road, Gitanga Close, Muthangari Gardens, Valley Arcade Shopping Centre, Othaya Road, Mararo Avenue, sehemu ya Argwings Kodhek, sehemu ya Oledume Road, sehemu ya Oloitoktok Road, sehemu ya Korosho Road na wateja wa karibu.
Nyandarua
Katika Kaunti ya Nyandarua, umeme utakatika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo ya Murungaru, Turasha, Memo, Engineer Town, Ndunyu Njeru, Karima Girls, Kinangop Dairy, Daima Dairy, Kaimba, Munyaka, Njabini, Sasumua Dam, Kinamba, Ndinda na maeneo ya karibu.
Nandi
Sehemu za Kaunti ya Nandi zitakosa umeme kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni, maeneo yaliyoathirika ni Cheptabach, Kibukwo, Kabirer, Maraba, Senetwo, Songhor, Soba River, Tachasis, Miteitei, Tinderet, Mbogo Valley na wateja jirani.
Vihiga
Umeme utakatika kutoka saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo ya Luanda Market, Ebwiranyi, Mukhalakhala, Epangá, Ebubayi, Mulele, Esaba, Esibila, Ebulondi, Esibakala, Radio Anyole, Radio Samaritan, Epali, Mabwi, Ebuyangu na maeneo ya karibu.
Tharaka Nithi
Katika Kaunti ya Tharaka Nithi, umeme utakatika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi alasiri katika Chera Market, Kanyuru Primary School, Ikawa Secondary, Gikumbo Village, Ngaani Primary School, Kamuguogo Primary School, Nyagakairu Primary School, Karamungi Secondary School na maeneo ya karibu.
Laikipia
Maeneo yatakayoathirika katika Kaunti ya Laikipia kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri ni Ol Pejeta, Depatas, Tundra, Freshigold, Segera, Zimbabwe, New Daraja Academy na maeneo jirani.
Meru
Baadhi ya maeneo ya Kaunti ya Meru yatakumbwa na katizo la umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Maeneo haya ni Kianjai Market, Ngundune Market, Michii Mikuru Tea Factory, KBC Nyambene, Kirema Kiuma AP Training, Kioro Market, Tigania Mission Hospital, Kamoja Road, Ntarami, Karii, Muutionjuri Dispensary, Mwerondu Market, Kadebe Dispensary na wateja jirani.
Kiambu
Sehemu za Kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni katika KIST, Mushroom East, Thindigua, Quickmart, GG Shopping Centre, Muthithi, Njathaini, Eden Ville na maeneo jirani.
Mombasa
Baadhi ya maeneo ya Kaunti ya Mombasa yatapata hitilafu ya umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathirika ni Coast Calcium, Waa Girls, Shonda Maweni na wateja jirani.
Kilifi
Katika Kaunti ya Kilifi, umeme utakatika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni katika maeneo ya Pwani University, Konjora, Palakumi, Ganze, Vitengeni, Matano Manne, Lango Baya, Magogoni na wateja jirani.
Kenya Power imetahadharisha wateja wake walioko katika maeneo haya kuchukua tahadhari zinazohitajika kwa ajili ya katizo hilo la umeme. Pia, imeahidi kufanya matengenezo kwa haraka ili kurejesha umeme katika maeneo husika ndani ya muda uliopangwa.
