Aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua Kiongozi wa Wiper bwana Stephine Kalonzo Musyoka na baadhi ya Wakenya wengi walionekana kutoa hisia na maoni tofauti
kuhusu michango ya Rais William Ruto Makanisani.
Rais Ruto kwa siku kadhaa zilizopita alionekana kutoa michango ya mamilioni katika
makanisa mbalimbali kama njia mojawapo ya kuonyesha ushirikiano baina ya
serikali na dini.
Juhudi hizi zinapoendelezwa na Rais kwa kutoa michango ya Harambe katika makanisa mbalimbali aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gathagua, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, baadhi ya Wakenya na viongozi wa dini kutoka sehemu tofauti za nchi walionekana kupinga mikakati hiyo ya Rais ya kuchangisha mamilioni walikosoa mpango huo wakiutaja kama kejeli na madharau na wengi wakisawiri kitendo hicho kama kicheko kwa Wakenya.
Mnamo Novemba 19,2024 katika kanisa la Katoliki la Soweto Kayole Rais alipohudhuria ibaada na
waumini wa dhehebu hilo aliweza kutoa
mchango wa kitita cha shilingi milioni mbili na laki sita 2.6m kwa ajili ya kujengea
mchungaji nyumba na kukamilisha ujenzi wa Kanisa.
Keshowe baada ya kanisa hilo kupokea mchango huo kutoka kwa
kiongozi wa taifa, Askofu Philip Anyolo anayesimamai
jimbo la Nairobi katika taarifa yake alisema kuwa walipokea sadaka ya mchango huo ila viongozi hawakueleza uhalisia wa michango hio hivyo ilikosa maadili basi hawakuwa na budi bali
kurudisha mchango huo.
Katika maelezo yao yaliosababisha kurudisha kwa hela hizo
taarifa ya Pamoja kulingana na mjibu wa Askofu Anyolo alikariri kwa kusema kuwa
kanisa liko huru na wazi kupokea matoleo na sadaka ambayo ni takatifu na ambayo
vyanzo vyake si vya kutiliwa shaka hivo maadili ni nguzo muhimu katika kila
mchango, michango ya aina hiyo ilikiuka
mswada wa kutoa michango wa mwaka wa 2024.
Mnamo Machi 3,2025 katika kanisa la Jesus Winners Ministry linaloongozwa
na Mhubiri Mwai kutoka Roysambu Rais alipohudhuria ibaada katika kanisa hilo
aliweza kutoa mchango wa shilingi milioni ishirini 20m na kuahidi kutoa mchango
mwingine katika Harambe wa shilingi milioni mia moja kwa ajili ya ujenzi wa
kanisa.
Isitoshe Jumapili ya Tarehe 9, Machi 2025 katika kanisa la
AIC Fellowship Annex Eldoret Rais
alipohudhuria ibaada aliweza kutoa mchango wa shilingi milioni ishirini 20m na
kuahidi kuendelea kutoa michango na kushiriki katika Harambe mbalimbali za
kuchangiza pesa.
Kutokana na huu msururu wa Rais kushiriki katika michango
mbalimbali viongozi mbalimbali Pamoja na Wakenya wengi wametilia shaka uhalali
wa pesa hizo wakihitaji uchunguzi wa dharura
kuanzishwa ili kubaini au kuweka wazi pale ambapo hela hizo hutoka ikikusudiwa
kuwa hali ya Uchumi na biashara ni mbaya kwa wakenya wengi.
Maoni tofauti kutoka kwa Wakenya walitoa wito kwa Rais wakimrai
aelekeze michango hiyo pia kwa wakenya walalahoi na kuwapa nafasi ya kujiunua
vilevile walisema pesa hizo zilifa kuelekezwa kwa Bima ya matibabu ya SHA ili
kutatau zogo la kutofanya kazi kwa kuwatibu wagonjwa hospitalini.