Mwakilishi wa kike wa Nairobi Bi Easther Passaris na mheshimiwa
ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya siasa Bi Juliah Chege kwa Pamoja waliwarai vijana kuwa watulivu na kutokubali
kugawanywa kwa misingi ya Kikabila na wanasiasa walio na maslahi ya binafsi.
Viongozi hao wakihojiwa katika kituo kimoja cha humu nchini walidadavua
wazi kuwa kuna hulka potovu miongoni kwa vijana ambayo imepandwa na baadhi ya
viongozi wanasiasa ili kuleta hali ya sintofahamu nchini.
Easther Passaris katika usemi wake aliweza kueleza kuwa ipo
haja ya kulea jamii iliyo na maadili kwanzia nyumbani ,kanisani ,shuleni
,vyuoni hadi katika viwango vya kuitwa wazazi wa siku za usoni.
Aliweza kusema kuwa serikali ilikuwa ikijitahidi kwa ajili
ya kuwatengenezea vijana ajira ambayo itawasaidia kukimu maisha ya siku zao za
usoni na kuwataka vijana waweze kuwa na mitazamo Chanya katika kazi na kwa
viongozi wao.
‘’Sasa hivi serikali inaendeleza mpango wa kuzindua vyanzo
vya kusomea masuala na teknologia kote nchini alimaaru ‘’computer hubs’’ kwa
hivyo ninarai vijana kuchukua fursa hio kupata elimu ya mitandaoni badala ya
kushinda kila wakati wakilalama na kupiga kelele’’ Passaris alisema.
Aliweza kufafanua kuwa ipo miradi mbalimbali ambayo serikali
inajitahidi ili kuhakikisha kuwa maisha ya vijana wetu inakuwa katika mkondo
mzuri kama vile kuwa na ajira ya kazi mtaaani ,ila akasema kuwa wapo
baadhi ya watu wengine wanaokosoa mpango huo kwa kuwachochea watu kutofanya
ilihali wao wana ajira.
Alisisitiza kuwa umoja na mshikamano wa nchi hupatikana ikiwa
kuna amani na utulivu ,iwapo viongozi wanashirikiana hiyo ni ishara kuwa
kutakuwa na maendeleo kila pembe ya nchi pasi kubaguliwa
Kwa upande wake bi Chege naye alirai vijana kutokubali
kuingizwa katika siasa za migawanyiko huku akiwaomba vijana kuwa imara kutetea
maslahi yao kwa kutumia njia za kisheria pasi kuzua fujo wala kuchanganywa na
viongozi ambao azma yao ni kutaka kuwagawanya vijana kwa misingi ya kikabila na
kuchochea ghasia .
Hata hivyo Bi Chege
aliweza kutoa wito kwa serikali kufanya hima ili kuwapa nafasi za ajira vijana
au nafasi mbalimbali ili kuepuka hilo joto la kisiasa ambalo linazidi kupanda
huku vijana wakikemea viongozi wa serikali kila uchao na kuwabandika majina
ambayo si mazuri wito sawia na huo uliweza kutolewa na Profesa Fred Ogola
ambaye ni kaimu mhadhiri mkuu chuo cha Strathmore.