Mkuu wa Kitengo cha Mazingira katika Kaunti ya Nairobi bwana
Geoffrey Mosiria alielezea sababu kuu
ambayo uhasama kati yake na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ulipoanzia.
Alipokuwa akihojiwa na kituo Kimoja nchini Bwana Mosiraa aliweza kufafanua kuwa
tofauti zao zilianza pale walipokuwa katika chuo kikuu cha Nairobi .
Alifafanua kuwa Mheshimiwa Babu kwa mara si moja ameishi kwa
misemo kuwa hamna siku ambayo atawahi kuja kushindwa au kuwa mtu kando na
kuwanianafasi ya kiti cha uongozi katika
chuo kikuu.
Bwana Mosira aliendelea na kusema kuwa alishindana na babu
Owino lakini aliibiwa Kura katika chuo kikuu cha Nairobi.
‘’Uhasama wangu na Babu ulitoka mbali ,Babu huwa anaamini
kuwa mimi sitawahi mshinda kwa vyovyote vile kando tu na kuwania siasa za
vyuoni ama sitawahi Kuwa chochote, Nilishindana na Babu katika kura za kusaka
uongozi chuo cha Naoirobi.
Kutokana na Babu kuwa alikuwa amejulikana na uongozi wa chuo sana aliweza kuibiwa kura na na kutangazwa mshindi aidha mkuu wa Kaunti ambaye amepata umaarua
mwingi katika Mitandao ya Kijamii kutokana na hatua yake ya kusuluhisha majanga yanayotokana na Mazingira .
Alifafanua akisema kuwa alisema kuwa Babu alimtafuta kumwarifu
kuwa alikuwa na azma ya kuwania kiti katika eneobunge la Embakasi Mashariki
mwaka wa 2017.
Kulingana na Mosira chama cha ODM kilimtaka asimame ili aweze
kutwaa ushindi wa chama hicho Alisema kuwa katika uchaguzi uliofuata vilevile
alimtafuta ambapo waliketi katika mkahawa mmoja sehemu za Kileleswa ili
kuzungumzia masuala ya siasa.
‘’Bwana Owino alinirai kwa sababu mimi ni binadamu nilimuelewa
na kumpa kibali cha kuendelea’’ Bwana Mosira aliendelea kufafanua kuwa huwa
anamwogopa akidhani kuwa huwa anadhani kuwa
anapana kuwa mpinzni wake mkuu katika
kinyan’ganyiro cha kusaka uongozi wa
eneo bunge la Embakasi Mashariki.
Bwana Mosira alionekana kumushauri Babu Kutekeleza wajibu
wake kama mbunge kwa kuhakisha kuwa anawapa wananchi waliomchagua maendeleo
ya kudumu na badala yake aache kuingilia
kazi za huduma za usafi wa Kaunti kwa kutuma takataka katika mitandao malimbali
ya kijamii kuashiria kuwa kazi haifanywi.