Otuoma ambaye alikuwa anazungumza baada ya kuhudhuria ibaada alionekana kumujibu mbunge wa Funyula oundo mudenyo baada ya kutilia shaka utenda kazi wake.
"Nataka kusema bwana Oundo, sisi hapa pesa tunapeana kwa wodi, ukieka words zote pamoja inashindana na yenye mnapata ya CDF. Sasa wakati mwingine hata mimi nashindwa, badala ya mwakilishi wadi kutembea akiambia wananchi nimepewa pesa fulani na kwa wodi yangu nafanya hii, wengine ni kuongea juu ya Gavana,' alisema Otuoma.
"Kwa mfano hiyo pesa uchukue kama hapa Samia kama ziko wadi nne, tayari hiyo ni milioni 80, pamoja na zile tunaongeza ni zaidi ya shilingi milioni 100. Pesa ambazo zinatoshana na za mgao wa Usitawi wa maeneobunge CDF. Sasa badala wewe useme umefanya nini kwa wadi yako, mbunge akisema amefanya nini na wewe pia unasema umefanya nini, " alieleza
Vile vile akizungumza amewataka wawakilishi wadi kuwa tayari kubeba msalaba wao siku ya kiama itakapofika iwapo watashindwa kueelezea wenyeji kile ambacho watakuwa wamekifanya kwa miaka mitano.
"Kila mtu kwa wodi yake atahesabu kazi yake wala sio kulaumu gavana, siku ya kiama ikifika kila mtu atajitetea. Kwa sababu nimepeana bilioni mia saba kwa wawakilishi wadi wote kwa pamoja na hizo ni pesa nyingi sana. Hakuna sheria ambayo inasema nafaa kuwapatia hiyo pesa. Mlifanya kampeni mkiahidi na tumewapea mtimize," aliweka wazi Otuoma.
Paul Otuoma ni gavana wa sasa na wa pili wa kaunti ya Busia.
Alichaguliwa kuwakilisha eneo bunge la Funyula katika Bunge la Kenya tangu uchaguzi mwaka 2007 na alikuwa waziri wa serikali za mitaa kuanzia 2010-2013. Alikuwa Mbunge wa Jimbo la Funyula hadi Agosti 2017.
Otuoma ni daktari wa mifugo aliyehitimu akishikilia Shahada ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi (1991), ambapo pia alipata MBA mnamo 2001.