
Maafisa wa Polisi katika kituo cha polisi cha Naivasha eneo la Naivasha walimkamata Jmshukiwa
kwa kwa madai ya kumiliki silaha hatari kinyume cha sheria.
Mshukiwa mwenye umri wa 30 alikamatwa na maafisa wa polisi kwa madai ya kumiliki Bunduki iliyokuwa na
marisasi mawili taarifa hizo ziliwafikia maafisa wa usalama kufuatia Habari kutoka
kwa raia.
Wakishughulikia Habari hizo kwa njia ya dharura maafisa
wa polisi waliari fiwa kuwa raia mmoja Aliona mshukiwa
mmoja akiwa amebeba marisasi katika baa
moja ya Nyama CHOMA kinamba Naivasha.
Maafisa wa usalama waliweza kuchukua hatua za upesi ili
kubaini na kumkamata mshukiwa kutoka mahali aliposemekana alikuwa bila kupoteza
muda wala kulimatia.
Kulingana na ukaguzi wa kina uliofanywa na maafisa wa
usalama wa kitengo cha DCI kuweza kutambua
aina ya silaha ambazo mshukiwa alikuwa nazo ni kuwa ilibainika wazi kuwa mshukiwa alikuwa
anamiliki bunduki ambayo ilikuwa na urefu wa milimita 7.62 na urefu wa marisasi
yenye milimita 9.
Mshukiwa alipatikana na silaha hizo haramu bila kuwa na vyeti au
vibali vya kumruhusu kumiliki silaha hizo na
alikuwa anakusudia kufanya nini nazo? Maswali yaliulizwa yakimkosa
majibu.
Mshukiwa baada ya kukamatwa alipelekwa katika kituo cha polisi cha Naivasha ambapo
uchunguzi wa kina unaendelea kumhusu mshukiwa
na baadaye ataweza kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka baada ya
uchunguzi kukamilika.
Maafisa wa DCI kwa
ushiriano na wananchi mara nyingi
wamekuwa macho na kuwahabarisha wananchi na kuwaarifu kuwa wawonapo jambo
lolote ambalo si sawa na ambalo
linatishia usalama wa taifa au wananchi wawe tayari kupiga ripoti kwa maafisa wa usalama kwa kutumia nambri ya simu
0800722203 bila malipo yoyote.
Kesi za wananchi kupatikanabna
silaha hatari bila vibali maalumu zimekuwa zikikithiri na kuchochea wasiwasi na
uwoga kwa wananchi huku wanaopatikana na silaha hizo wakikosa kufafanuani wapi
wanakopta silaha hizi haramu ambazo serikali instahili iwe na uwezo kwa
kufahamu ni akina nani wanaomiliki silaha
hizo.
Juhudi za maafisa wa usalama kufanya bidii na juhudi za
upesi kumkamata bwana Matu ni jambo ambalo linastahiki kupongezwa kwa dhati kuu
ikizingatiwa kuwa kama mshukiwa huyo hangetambuliwa kutoka kwa wananchi angekuwa
ni mwiba mkubwa sana kwa usalama wa wananchi kwa jumla.