
Mvua inatarajiwa kuendelea kunyesha katika maeneo kadhaa ya hapa nchini hili ni kulingana na utabiri uliyotolewa na idara ya utabiri wa hali ya hewa.
Baadhi ya maeneo ambayo yatashuhudia matukio ya mvua kubwa yanalenga maeneo ya Nyanda za Juu Mashariki na Magharibi mwa Bonde la Ufa, Bonde la Ziwa Victoria, nyanda za chini za kusini-mashariki na kaskazini mashariki mwa Kenya.
Leo tarehe 19 machi na siku tatu zijazo baadhi ya sehemu ambazo sitashuhudia mvua kubwa ikiandamana na ngurumo za radhi nyakati za jioni zitahusisha maeneo ya bonde la ufa, bonde la ziwa Victoria, na nyanda za Juu magharibi mwa bonde la Ufa.
Sehemu hizi sinahusu kauniti zifuatazo, (Siaya, Kisumu, Homabay, Migori, Kisii, Nyamira, Trans Nzoia, Baringo, Uasin Gishu, Elgeyo-Marakwet, Nandi, Nakuru, Narok, Kericho, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Busia and West Pokot.
Baadhi ya sehemu hizo pia zitashuhudia mvua ya rasharasha nyakati za asubuhi na jioni.
Nyanda za juu mashariki mwa Bonde la Ufa [ ikiwa ni pamoja na Kaunti ya Nairobi, Nyandarua, Laikipia, Nyeri,Kirinyaga, Murang'a, Kiambu, Meru, Embu na Tharaka] zitashuhudia mvua chache nyakati za asubuhi ila wakati wa jioni kutakuwa na mvua kubwa ikiandamana na ngurumo za radi. Wakati wa usiku kutakuwa asilimia ndogo sana ya mvua na wingu zito.
Kaunti za kaskazini-mashariki ambazo ni pamoja na Marsabit,Wajir, Garissa, Isiolo na Mandera zitashuhudia mvua ya kadri nyakati za asubuhi isipokuwa siku ya jumapili ambako kutashuhudiwa jua.
Wakati wa usiku katika maeneo haya kutakuwa na mvua chache lakini leo na kesho jioni baadhi ya sehemu hizi zitashuhudia mvua kubwa ikiandamana na ngurumo za radi.
Kaskazini-Magharibi ambayo inahusisha kaunti mbili za Turkana na Samburu zitashuhudia jua na mawingu mazito kwa siku chache mbele isipokuwa leo nyakati za jioni ambako kunatarajiwa mvua kubwa ikiandamana na ngurumo za radi.