Huduma ya kitaifa kwa polisi(NPS) ilitoa na kuelezea mikakati
ya usalama ambayo imewekwa kufuatia mashindanao ya WRC Safari Rally 2025 ambayo
yanang;oa nanga Alhamisi ya tarehe 20/03/2025 hadi Jumapili 23/03/2025 mjini
Naivasha.
Katika ujumbe wake kwa mtandao wa X huduma ya polisi
iliweza kuwarai wananchi kuzingatia masharti yote ambayo yamewekwa pamoja na
kushirikiana na polisi kufanikisha usalama wa kila mmoja.
Baadhi ya maagizo yaliyotolewa na huduma ya kitafa kwa
polisi ni matumizi ya barabara mbadala ambazo umma utaambiwa kuelezewa
kuzitumia vilevile kuwepo kwa maafisa wa
trafiki katika Barabara zote ili
kuhakikisha kuwa kuna usafiri mwema bila
matata.
Hata hivyo huduma hiyo ya polisi ilisema kuwa kwa ushirikiano
na huduma ya kitaifa ya usafiri barabarani (NTSA) itahakikisha kuwa kila kitu kinaendeshwa jinsi
kilivyoratibiwa pasi shida yoyote.
Huduma hiyo iliweza kushauri umma kuzinggatia maagizo na
utaratibu wote uliowekwa na asasi za kiusalama na kushauri umma kuripoti visa
vyovyote vinavyotishia usalama wa wananchi.
Madereva wa mabasi na malori waliweza kushauriwa
kutoegesha magari yao kando ya Barabara kuu ya Naivasha- Nakuru kwa ajili ya kutotatiza usalama mwema,
watumizi wa Barabara kwa njia ya kusari kwa miguu na pikipiki pia waliombwa wawe
wangalifu zaidi.
Huduma hiyo kwa polisi iliweza kutoa nambari za simu kwa
umma na kutangaza wazi kuwa iwapo kunaweza kutokea jambo lisilo la kawaida au
kutaka kuarifu umma bila shaka nambari za simu zilikuwa wazi kama ifuatavyo, nambari
ya polisi bila malipo ni 099911112 au Fichu
na DIC 0800722203.
Kando na usalama pia mashindano hayo hayazungumzii tu
burudani pekee bali pia ni kitega Uchumi kikuu kwa wakaazi wa eneo la Naivasha na viunga vyake Pamoja na
serikali kwa jumla kwani Mashindano hayo yataweza kuwavutia watalii wengi nchini
ambao wataleta fedha nyingi kwa taifa.
Vilevile mikahawa mbalimbali na wafanyakazi watakaofanya
kazi katika hoteli mbalimbali watanufaika
na kujenga viwango vyao vya kimapato.
Mashindano ya Safari rally huweza kuwavutia takribani wageni
elfu 100,000 na hutazamwa na watu katika vyombo vya Habari milioni 120 katika
jumla ya mataifa 170 duniani na zaidi ya runinga 50 za kimataifa ambazo
hupeperusha hewani mashindano hayo.