Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen alimhakikishia
mamake mvulana aliyetoweka kwa jina Brian Odhiambo kuwa haki itapatikana.
Alipokuwa akizungumza naye Bi Elizabeth Auma mkaazi wa Nakuru,
mnamo Jumatano Machi 19,2025 ambapo alimhakikishai kuwa haki itapatikana kwa jamaa
na familia ya Brian aliyetoweka katika ziwa Nakuru.
‘’Nikirudi Nairobi nitaketi
na wale ambao walikuwa wanafanya uchunguzi waniambie uchunguzi ulifikia wapi? Lakini
nia yangu ni kuhakikisha kuwa mwishowe
umepata haki .Nitalichukulia hili suala kama langu ila chenye ninaweza sema tu
ni kuwa pole kwako na kwa jamii yako ila
haki itapatikana’’ Murkomen alisema.
Hilo lilitokea baada ya Bi Auma kukatiza hotuba ya Murkomen
alipokuwa kule Shabab Nakuru Magharibi katika hafla ya kuzindua kampeni ya
kitaifa ya watu kujisajili kupata vitambulisho vya taifa.
Murkomen aliweza kuwaamuru maafisa wake wa usalama
kumuruhusu aseme naye hio ni baada ya kushangiliwa na umati wa watu kwa ujasiri huo alioonyesha. Baadaye Waziri aliweza kumwalika Bi Auma
katika afisi za halimashauri ya Kaunti
ili aeleze kwa kina kilichojiri kuhusu mwanawe.
Auma alimurai Waziri aweze kumsaidia kupata kule mwili wa
mwanawe ulipo,alimurai Waziri kwa masikitiko makubwa.
‘’Maafisa wote waliohusika katikla tukio hilo
watafikishwa kortini na watapoteza kazi zao. Kuna wakenya wengi waliotoweka
kama Brian ni mamake tu Brian ambaye amenifikia na kunitarifu kuhusu kutoweka
kwa mwanawe, ningependa kuwaarifu kuwa niko imara na wewe na nitafanya kila juhudi
kuhakikisha kuwa wale maafisa wa KWS waliohusika watatuambia Brian yuko wapi’’
Waziri Murkomen alisema.
‘’Tumeshuhudia baadhi ya maafisa wa KWS wakihusika katika
biashara ya uuzaji Samaki ndani ya ziwa Nakuru wakati ambapo wakenya wengine wanapokuja
kufanya shughuli za biashara hapo wanateswa na kunyanyaswa na maafisa hao’’ Waziri
alieleza.
Brian Odhiambo aliripotiwa kupotea mnamo tarehe 18
Januari,2025 akiwa karibu na kampuni ya KWS upande wa ziwa Nakuru
alipoonekana mwisho.
Baada ya juma moja mahakama ya Nakuru iliamuru afisa msimamizi
wa mbuga ya wanyamapori ya Nakuru atoe mwili
wa Brian akiwa hai au maiti.
Mnamo Jumanne Machi 18,2025 Wakili wa familia ya Odhiambo
na wanaharakati waliruhusiwa ndani ya mbuga ambapo walikisia kuwa mwili wa Brian
ulikuwa umezikwa na hivyo haungeonekana.
‘’Makaburi yote yanaonekana yamechimbuliwa na miili kutolewa ila nina uhakika na matumaini