logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maraga akubali wito wa vijana wa Gen Z wa kuwania Urais 2027

Aliyekuwa Jaji mkuu David Maraga alikubali wito wa vijana wa kizazi cha Gen Z kwa kuitikia wito wa kumtaka kuwania urais mwaka wa 2027

image
na Evans Omoto

Yanayojiri28 March 2025 - 07:34

Muhtasari


  • Alizungumza akiwa katika  Kaunti ya Migori Katika chuo kikuu cha Rongo baada ya kuwahutubia wanafunzi kuhusu maswala mabalimbali yanayofungamana na uongozi. 
  • Jaji huyo mkuu wa Zamani alieleza kuelezea ari yake kuwa angependa tena  kuongoza mhimili mwingine wa serikali kama alivyoongoza mahakamani kama jaja mkuu kwa miaka minne na miezi mitatu tangu mwaka wa 2016-2021.

Aliyekuwa Jaji mkuu David Maraga alikubali wito wa vijana wa kizazi  cha  Gen Z kwa  kuitikia wito wa kumtaka kuwania  urais mwaka wa 2027.

Alizungumza akiwa katika  Kaunti ya Migori Katika chuo kikuu cha Rongo baada ya kuwahutubia wanafunzi kuhusu maswala mabalimbali yanayofungamana na uongozi. 

Jaji huyo wa Zamani aliweza kuelezea ari yake kuwa angependa tena  kuongoza mhimili mwingine wa serikali kama alivyoongoza mahakamani kama jaja mkuu kwa miaka minne na miezi mitatu tangu mwaka wa 2016-2021.

''Nimehudumu  mwanzoni kama Jaji mkuu katika jamuhuri ya Kenya kwa  hivyo sioni kama kuna ubaya  wowote mimi kuongoza mhimili mwingine wa serikali  kwa kuwa ni jambo zuri tena lenye tija katika  taifa  na kwa wananchi" Maraga alisema.

Kulingana na mujibu wa  maelezo yake Bwana Maraga  alionyesha  kuwa na  uzoevu katika masuala ya uongozi hivyo alikuwa na imani fika iwapo angepewa fursa ya kuliongoza taifa  bila shaka  angetekeleza wajibu huo  kwa kujitolea na kwa kuzingatia mwongozo wa katiba.

Hata hivyo aliweza kukosoa serikali iliyoko mamalakani kwa kuweza  kuunda  bajeti ya  taifa ambayo ni fisadi na  ambayo haioani na malengo wala mahitaji ambayo Wakenya  wanatilia kipaumbele.

Alisuta wale ambao huunda na kukadiria bajeti ya  taifa kwa kutotengea masuala muhimu pesa na kuangazia  masuala ambayo mwananchi  mlipa ushuru anakabiliwa nayo na  badala yake bajeti huundwa kwa  kuelekezea pesa nyingi kwa vitu ambavyo si vya muhimu sana  kwa mawananchi mlipa ushuru.

''Kwa sasa ninafanya ushirikiano na washikadau mbalimbali ili kuweza kufanya  tangazo rasmi kwa wananchi kuhusu msimamamo ambao nitakuwa nimeamua  lakini kile ambacho ninashutumu kwa kusema kuwa ni tatizo kubwa nchini  ni usfisadi  na kukuwa na  taasisi nchini ambazo ni fisadi''. Maraga .alisema.

Hata katika usanjari huo aliweza kuwarai wakenya kuishi kwa amani  na kuwa  katika mstari wa mbele kuwajibikia  vitendo  vyao na  vilevile kuonyesha mifano  miema katiaka uongozi  wao.

David si wa  kwanza kutoka jimbo la Kisii ambaye  ameonyesha ari ya  kuwania kiti cha urais nchini aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani Daktari Fred Matingi na Mwanaharakati Morara Kebaso ni miongoni mwa  viongozi  ambao wameonyesha ari ya kuwania kiti cha Urais mwaka wa 2027 hata hivyo bwana Maraga anakumbuwa na wengi kwa kuwa jaji wa kwanza kufutilia mbali matokeo ya urais ya mwaka wa 2017.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved